1 Chronicles 1:43 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wafuatao ndio wafalme waliotawala nchi ya Edomu kabla mfalme yeyote hajatawala Waisraeli: Bela mwana wa Beori alitawala nchi ya Edomu, akiwa na makao yake makuu katika mji wa Dinhaba.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hawa ndio wafalme waliotawala Edomu kabla hajatawala mfalme yeyote wa Waisraeli: Bela mwana wa Beori, ambaye mji wake ni Dinhaba.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi hawa ndio wafalme waliomiliki katika nchi ya Edomu, kabla hajamiliki mfalme awaye yote juu ya wana wa Israeli; Bela, mwana wa Beori; na jina la mji wake ni Dinhaba.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wafuatao ndio wafalme waliotawala nchi ya Edomu kabla mfalme yeyote hajatawala Waisraeli: Bela mwana wa Beori alitawala nchi ya Edomu, akiwa na makao yake makuu katika mji wa Dinhaba.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hawa ndio wafalme waliotawala Edomu kabla hajatawala mfalme ye yote wa Waisraeli: Bela mwana wa Beori, ambaye mji wake ni Dinhaba.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hawa ndio wafalme waliotawala Edomu kabla hajatawala mfalme yeyote wa Waisraeli: Bela mwana wa Beori, ambaye mji wake ni Dinhaba.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi hawa ndio wafalme waliotawala katika nchi ya Edomu, kabla hajatawala mfalme yeyote juu ya wana wa Israeli; Bela, mwana wa Beori; na jina la mji wake ni Dinhaba.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wafuatao ndio wafalme waliotawala nchi ya Edomu kabla mfalme yeyote hajatawala Waisraeli: Bela mwana wa Beori alitawala nchi ya Edomu, akiwa na makao yake makuu katika mji wa Dinhaba.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao hawa ndio wafalme walioshika ufalme katika nchi ya Edomu, wana wa Isiraeli walipokuwa hawajapata bado mfalme: Bela, mwana wa Beori; nalo jina la mji wake ni Dinihaba.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi hawa ndio wafalme waliomiliki katika nchi ya Edomu, kabla hajamiliki mfalme awaye yote juu ya wana wa Israeli; Bela, mwana wa Beori; na jina la mji wake ni Dinhaba.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hawa ndio wafalme waliotawala katika inchi ya Edomu mbele mufalme yeyote hajatawala Waisraeli: Bela mwana wa Beori, akiwa na makao yake makubwa katika muji wa Dinihaba. Yobabu mwana wa Zera kutoka muji wa Boza. Husamu wa inchi ya Watani. Hadadi mwana wa Bedadi, makao yake makubwa yakiwa katika muji wa Awiti. Huyu ndiye aliyepiga na kushinda Wamidiani katika inchi ya Moabu. Samula kutoka muji wa Masireka. Saulo kutoka muji wa Rehoboti unaokuwa, karibu na muto Furati. Bali-Hanani mwana wa Akibori. Hadadi kutoka muji wa Pai. Jina la muke wake ni Mehetabeli, binti ya Matiredi na mujukuu wa Mesahabu.