1 Chronicles 10:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
mashujaa wote waliondoka na kuuchukua mwili wa Shauli na miili ya wanawe, wakaileta mpaka Yabeshi. Wakaizika mifupa yao chini ya mwaloni huko Yabeshi, nao wakafunga kwa muda wa siku saba.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
mashujaa wao wote wakaondoka, wakautwaa mwili wa Sauli na miili ya wanawe, wakaileta Yabeshi. Wakaizika mifupa yao chini ya mwaloni ulio Yabeshi, nao wakafunga kwa siku saba.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
wakainuka mashujaa wote, wakautwaa mwili wake Sauli, na miili ya wanawe, wakaileta Yabeshi, wakaizika mifupa yao chini ya mwaloni huko Yabeshi, nao wakafunga muda wa siku saba.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
mashujaa wote waliondoka na kuuchukua mwili wa Shauli na miili ya wanawe, wakaileta mpaka Yabeshi. Wakaizika mifupa yao chini ya mwaloni huko Yabeshi, nao wakafunga kwa muda wa siku saba.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
mashujaa wote wakaondoka, wakautwaa mwili wa Sauli na miili ya wanawe, wakaileta Yabeshi. Wakaizika mifupa yao chini ya mti mkubwa huko Yabeshi, nao wakafunga kwa siku saba.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
mashujaa wao wote wakaondoka, wakautwaa mwili wa Sauli na miili ya wanawe, wakaileta Yabeshi. Wakaizika mifupa yao chini ya mti mkubwa huko Yabeshi, nao wakafunga kwa siku saba.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
wakainuka mashujaa wote, wakautwaa mwili wake Sauli, na miili ya wanawe, wakaileta Yabeshi, wakaizika mifupa yao chini ya mwaloni huko Yabeshi, nao wakafunga muda wa siku saba.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
mashujaa wote waliondoka na kuuchukua mwili wa Shauli na miili ya wanawe, wakaileta mpaka Yabeshi. Wakaizika mifupa yao chini ya mwaloni huko Yabeshi, nao wakafunga kwa muda wa siku saba.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
wakaondoka watu wote walioweza kupiga vita, wakauchukua mzoga wa Sauli, nayo mizoga ya wanawe, wakaipeleka Yabesi, wakaizika mifupa yao chini ya mkwaju kwao Yabesi, wakafunga mfungo siku saba.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
wakainuka mashujaa wote, wakautwaa mwili wake Sauli, na miili ya wanawe, wakaileta Yabeshi, wakaizika mifupa yao chini ya mwaloni huko Yabeshi, nao wakafunga muda wa siku saba.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
mashujaa wote wakaondoka na kutwaa mwili wa Saulo na miili ya wana wake, wakaileta mpaka Yabesi. Wakazika mifupa yao chini ya muti wa mwalo kule Yabesi, nao wakafunga kula kwa muda wa siku saba.