1 Chronicles 10:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndipo Shauli alipomwambia mtu aliyembebea silaha, “Chomoa upanga wako unichome nife, ili watu hawa wasiotahiriwa wasije wakanidhihaki.” Lakini huyo aliyembebea silaha hakuthubutu; kwa sababu aliogopa sana. Hivyo, Shauli alichukua upanga wake mwenyewe akauangukia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sauli akamwambia mbeba silaha wake, “Futa upanga wako unichome nao, la sivyo hawa watu wasiotahiriwa watakuja na kunidhalilisha.” Lakini mbeba silaha wake akaogopa sana wala hakuweza kufanya hivyo. Kwa hiyo Sauli akachukua upanga wake mwenyewe na kuuangukia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo Sauli akamwambia yule mchukua silaha zake, Futa upanga wako, unichome nao, wasije watu hawa wasiotahiriwa wakanisimanga. Lakini huyo mchukua silaha zake akakataa; kwa sababu aliogopa sana. Basi Sauli akautwaa upanga wake, akauangukia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndipo Shauli alipomwambia mtu aliyembebea silaha, “Chomoa upanga wako unichome nife, ili watu hawa wasiotahiriwa wasije wakanidhihaki.” Lakini huyo aliyembebea silaha hakuthubutu; kwa sababu aliogopa sana. Hivyo, Shauli alichukua upanga wake mwenyewe akauangukia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sauli akamwambia mbeba silaha wake, “Futa upanga wako unichome, la sivyo hawa watu wasiotahiriwa watanidhalilisha.” Lakini yule mbeba silaha wake akaogopa sana wala hakuthubutu kufanya hivyo. Kwa hiyo Sauli akachukua upanga wake akajichoma mwenyewe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sauli akamwambia mbeba silaha wake, “Futa upanga wako unichome nao, la sivyo hawa watu wasiotahiriwa watakuja na kunidhalilisha.” Lakini mbeba silaha wake akaogopa sana wala hakuweza kufanya hivyo. Kwa hiyo Sauli akachukua upanga wake mwenyewe na kuuangukia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo Sauli akamwambia yule mchukua silaha zake, Futa upanga wako, unichome nao, ili watu hawa wasiotahiriwa wasije wakanisimanga. Lakini huyo mchukua silaha zake akakataa; kwa sababu aliogopa sana. Basi Sauli akautwaa upanga wake, akauangukia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndipo Shauli alipomwambia mtu aliyembebea silaha, “Chomoa upanga wako unichome nife, ili watu hawa wasiotahiriwa wasije wakanidhihaki.” Lakini huyo aliyembebea silaha hakuthubutu; kwa sababu aliogopa sana. Hivyo, Shauli alichukua upanga wake mwenyewe akauangukia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Sauli alipomwambia mchukua mata yake: Uchomoe upanga wako, unichome nao, hao wasiotahiriwa wasije kunichezea vibaya! Mchukua mata yake alipokataa kwa kuogopa sana, Sauli akausimika upanga, akauangukia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo Sauli akamwambia yule mchukua silaha zake, Futa upanga wako, unichome nao, wasije watu hawa wasiotahiriwa wakanisimanga. Lakini huyo mchukua silaha zake akakataa; kwa sababu aliogopa sana. Basi Sauli akautwaa upanga wake, akauangukia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo Saulo akamwambia mutu aliyemubebea silaha: “Chomoa upanga wako unichome nikufe, kusudi watu hawa wasiotahiriwa wasikuje kunichekelea.” Lakini yule aliyemubebea silaha hakutaka kufanya vile; aliogopa sana. Halafu, Saulo alitwaa upanga wake mwenyewe akauangukia.