1 Chronicles 11:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hii ndiyo orodha ya wakuu wa mashujaa wa Daudi, ambao pamoja na watu wengine wote wa Israeli, walimuunga mkono kwa pamoja ili awe mfalme, sawa na neno la Mwenyezi-Mungu alilotoa juu ya Waisraeli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hawa walikuwa wakuu wa mashujaa wa Daudi: wao pamoja na Waisraeli wote wakauimarisha ufalme wake ili kuenea katika nchi yote, sawasawa na neno la Mwenyezi Mungu aliloahidi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi hawa ndio wakuu wa mashujaa aliokuwa nao Daudi, waliojitia nguvu pamoja naye katika ufalme wake, pamoja na Israeli wote, ili kumfanya awe mfalme, sawasawa na neno la Bwana alilonena juu ya Israeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hii ndiyo orodha ya wakuu wa mashujaa wa Daudi, ambao pamoja na watu wengine wote wa Israeli, walimuunga mkono kwa pamoja ili awe mfalme, sawa na neno la Mwenyezi-Mungu alilotoa juu ya Waisraeli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hawa ndio waliokuwa wakuu wa mashujaa wa Daudi: wao pamoja na Israeli wote, wakauimarisha ufalme wake ili kuenea katika nchi yote, kama BWANA alivyoahidi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hawa ndio waliokuwa wakuu wa mashujaa wa Daudi: wao pamoja na Israeli wote wakauimarisha ufalme wake ili kuenea katika nchi yote, kama bwana alivyoahidi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi hawa ndio wakuu wa mashujaa aliokuwa nao Daudi, waliojitia nguvu pamoja naye katika ufalme wake, pamoja na Israeli wote, ili kumfanya awe mfalme, sawasawa na neno la BWANA alilonena juu ya Israeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hii ndiyo orodha ya wakuu wa mashujaa wa Daudi, ambao pamoja na watu wengine wote wa Israeli, walimuunga mkono kwa pamoja ili awe mfalme, sawa na neno la Mwenyezi-Mungu alilotoa juu ya Waisraeli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hawa ndio wakuu wao mafundi wa vita, Dawidi aliokuwa nao, waliomsaidia kwa nguvu zao, apate ufalme; nao Waisiraeli wote walikuwa upande wao, walipomfanya kuwa mfalme, kama Bwana alivyowaambia Waisiraeli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi hawa ndio wakuu wa mashujaa aliokuwa nao Daudi, waliojitia nguvu pamoja naye katika ufalme wake, pamoja na Israeli wote, ili kumfanya awe mfalme, sawasawa na neno la BWANA alilonena juu ya Israeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Haya ndiyo majina ya wakubwa wa mashujaa wa Daudi, ambao pamoja na watu wengine wote wa Israeli, walimwunga mukono kwa pamoja kusudi akuwe mufalme, sawa na neno Yawe alilotoa juu ya Waisraeli.