1 Chronicles 11:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku moja Eleazari alikuwa pamoja na Daudi huko Pas-damimu, wakati Wafilisti walipokusanyika kupigana vita. Huko kulikuwa na shamba lenye shayiri tele, nao Waisraeli walikuwa wamewakimbia Wafilisti.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Huyo alikuwa pamoja na Daudi huko Pas-Damimu, wakati Wafilisti walikusanyika huko kwa ajili ya vita. Mahali palipokuwa na shamba limejaa shayiri, vikosi vya Israeli vikawakimbia Wafilisti.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Huyo alikuwa pamoja na Daudi huko Pasdamimu; ndiko Wafilisti walikokusanyika vitani,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku moja Eleazari alikuwa pamoja na Daudi huko Pas-damimu, wakati Wafilisti walipokusanyika kupigana vita. Huko kulikuwa na shamba lenye shayiri tele, nao Waisraeli walikuwa wamewakimbia Wafilisti.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Huyo alikuwa pamoja na Daudi huko Pas-Damimu, wakati Wafilisti walipokusanyika huko kwa ajili ya vita. Huko ambapo kulikuwa na shamba lililokuwa limejaa shayiri, vikosi vya Israeli vikawakimbia Wafilisti.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Huyo alikuwa pamoja na Daudi huko Pas-Damimu, wakati Wafilisti walikusanyika huko kwa ajili ya vita. Huko ambapo kulikuwa na shamba lililokuwa limejaa shayiri, vikosi vya Israeli vikawakimbia Wafilisti.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Huyo alikuwa pamoja na Daudi huko Pasdamimu; ndiko Wafilisti walikokusanyika vitani, palipokuwa na shamba lililojaa shayiri; na hao watu wakakimbia mbele ya Wafilisti.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku moja Eleazari alikuwa pamoja na Daudi huko Pas-damimu, wakati Wafilisti walipokusanyika kupigana vita. Huko kulikuwa na shamba lenye shayiri tele, nao Waisraeli walikuwa wamewakimbia Wafilisti.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Huyu alikuwa pamoja na Dawidi huko Pasi-Damimu, Wafilisti walipokusanyika huko kupigana naye. Huko kulikuwa na kipande cha shamba lenye mawele; hapo, watu walipowakimbia Wafilisti,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Huyo alikuwa pamoja na Daudi huko Pasdamimu; ndiko Wafilisti walikokusanyika vitani, palipokuwa na konde limejaa shayiri; na hao watu wakakimbia mbele ya Wafilisti.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku moja Eleazari alikuwa pamoja na Daudi kule Pasi-Damimu, wakati Wafilistini walipokusanyika kupigana vita. Kule kulikuwa shamba lenye shayiri tele, lakini Waisraeli wakawakimbia Wafilistini.