1 Chronicles 11:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Daudi na Eliazari walisimama imara katikati ya shamba hilo ili kulitetea, wakawaua Wafilisti; Mwenyezi-Mungu akawaokoa kwa kuwapa ushindi mkubwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Eleazari na Daudi wakasimama imara katikati ya lile shamba, nao wakalishindania na kuwaua Wafilisti. Naye Mwenyezi Mungu akawapa ushindi mkubwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo hao wakasimama katikati ya konde lile, wakalipigania, wakawaua Wafilisti; naye Bwana akafanya wokovu mkuu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Daudi na Eliazari walisimama imara katikati ya shamba hilo ili kulitetea, wakawaua Wafilisti; Mwenyezi-Mungu akawaokoa kwa kuwapa ushindi mkubwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini Eleazari na Daudi wakasimama imara katikati ya lile shamba, nao wakalishindania na wakawaua Wafilisti. Naye BWANA akawapa ushindi mkubwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Eleazari na Daudi wakasimama imara katikati ya lile shamba, nao wakalishindania na wakawaua Wafilisti. Naye bwana akawapa ushindi mkubwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo hao wakasimama katikati ya shamba lile, wakalipigania, wakawaua Wafilisti; naye BWANA akafanya wokovu mkuu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Daudi na Eliazari walisimama imara katikati ya shamba hilo ili kulitetea, wakawaua Wafilisti; Mwenyezi-Mungu akawaokoa kwa kuwapa ushindi mkubwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
ndipo, hawa walipokuja kusimama katikati ya hicho kipande cha shamba, wakakiponya wakiwapiga wafilisti; ndivyo, Bwana alivyowaokoa na kuwapatia wokovu mkubwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo hao wakasimama katikati ya konde lile, wakalipigania, wakawaua Wafilisti; naye BWANA akafanya wokovu mkuu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini wakasimama imara katikati ya shamba lile kwa kulikinga, wakaua Wafilistini; Yawe akawaokoa kwa kuwapa ushindi mukubwa.