1 Chronicles 11:18 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wale mashujaa wake watatu walitoka, wakapenya katikati ya kambi ya jeshi la Wafilisti, wakaenda na kuchota maji katika kisima cha Bethlehemu, karibu na lango la mji, wakamletea Daudi. Lakini Daudi akakataa kuyanywa, na badala yake akayamwaga chini kama tambiko kwa Mwenyezi-Mungu
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hivyo wale watatu, wakapita katikati ya safu za Wafilisti, wakachota maji kutoka kwa kisima kilicho karibu na lango la Bethlehemu, wakamletea Daudi. Lakini yeye akakataa kuyanywa. Badala yake, aliyamimina mbele za Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi hao watatu wakapenya jeshi la Wafilisti, wakateka maji kutoka kile kisima cha Bethlehemu, kilicho karibu na lango, wakayachukua, wakamletea Daudi; walakini Daudi hakukubali kuyanywa, akayamimina mbele za Bwana;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wale mashujaa wake watatu walitoka, wakapenya katikati ya kambi ya jeshi la Wafilisti, wakaenda na kuchota maji katika kisima cha Bethlehemu, karibu na lango la mji, wakamletea Daudi. Lakini Daudi akakataa kuyanywa, na badala yake akayamwaga chini kama tambiko kwa Mwenyezi-Mungu
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hivyo wale watatu, wakapita katikati ya safu za Wafilisti, wakachota maji kutoka kwenye hicho kisima kilichoko nje ya lango la Bethlehemu, wakamletea Daudi. Lakini yeye akakataa kuyanywa. Badala ya kuyanywa akayamimina mbele za BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hivyo wale watatu, wakapita katikati ya safu za Wafilisti, wakachota maji kutoka kwa kisima kilicho karibu na lango la Bethlehemu, wakamletea Daudi. Lakini yeye akakataa kuyanywa. Badala yake, aliyamimina mbele za bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi hao watatu wakapenya jeshi la Wafilisti, wakateka maji kutoka kile kisima cha Bethlehemu, kilicho karibu na lango, wakayachukua, wakamletea Daudi; lakini Daudi hakukubali kuyanywa, akayamimina mbele za BWANA;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wale mashujaa wake watatu walitoka, wakapenya katikati ya kambi ya jeshi la Wafilisti, wakaenda na kuchota maji katika kisima cha Bethlehemu, karibu na lango la mji, wakamletea Daudi. Lakini Daudi akakataa kuyanywa, na badala yake akayamwaga chini kama tambiko kwa Mwenyezi-Mungu
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, wale watatu walipojipenyeza makambini mwa Wafilisti, wakachota maji katika kisima cha Beti-Lehemu kilichoko langoni, wakayachukua, wakamletea Dawidi, lakini Dawidi hakutaka kuyanywa, akammwagia Bwana kuwa kinywaji cha tambiko,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi hao watatu wakapenya jeshi la Wafilisti, wakateka maji kutoka kile kisima cha Bethlehemu, kilicho karibu na lango, wakayachukua, wakamletea Daudi; walakini Daudi hakukubali kuyanywa, akayamimina mbele za BWANA;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wale mashujaa wake watatu wakatoka, wakapenya katikati ya kambi ya jeshi la Wafilistini, wakaenda na kuchota maji katika kisima cha Betelehemu, karibu na mulango wa muji, wakamuletea Daudi. Lakini Daudi akakataa kuyakunywa, na kwa pahali pake akayamwanga chini kama sadaka kwa Yawe