1 Chronicles 11:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo awali, Shauli alipokuwa mfalme wewe ndiwe uliyewaongoza Waisraeli vitani, na Mwenyezi-Mungu, Mungu wako alikuambia, ‘Utakuwa mchungaji wa watu wangu Israeli, na utakuwa mkuu wa watu wangu Israeli.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Zamani, wakati Sauli alikuwa mfalme, wewe ndiwe uliyeiongoza Israeli vitani, naye Mwenyezi Mungu, Mungu wako, alikuambia, ‘Wewe utawachunga watu wangu Israeli, na utakuwa mtawala wao.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Katika zamani za kale, hata hapo Sauli alipokuwa mfalme, wewe ndiwe uliyewatoa na kuwaingiza Israeli. Naye Bwana, Mungu wako, akakuambia, Ndiwe, utakayewalisha watu wangu Israeli, ndiwe utakayekuwa mkuu juu ya watu wangu Israeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo awali, Shauli alipokuwa mfalme wewe ndiwe uliyewaongoza Waisraeli vitani, na Mwenyezi-Mungu, Mungu wako alikuambia, ‘Utakuwa mchungaji wa watu wangu Israeli, na utakuwa mkuu wa watu wangu Israeli.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati wote uliopita, hata wakati Sauli alipokuwa mfalme, wewe ndiwe uliyeiongoza Israeli vitani, naye BWANA Mungu wako alikuambia, ‘Wewe utawachunga watu wangu Israeli, na utakuwa mtawala wao.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Zamani, wakati Sauli alikuwa mfalme, wewe ndiwe uliyeiongoza Israeli vitani, naye bwana Mwenyezi Mungu wako alikuambia, ‘Wewe utawachunga watu wangu Israeli, na utakuwa mtawala wao.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Katika zamani za kale, hata hapo Sauli alipokuwa mfalme, wewe ndiwe uliyeongoza jeshi la Israeli. Naye BWANA, Mungu wako, akakuambia, Ndiwe, utakayewalisha watu wangu Israeli, ndiwe utakayekuwa mkuu juu ya watu wangu Israeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo awali, Shauli alipokuwa mfalme wewe ndiwe uliyewaongoza Waisraeli vitani, na Mwenyezi-Mungu, Mungu wako alikuambia, ‘Utakuwa mchungaji wa watu wangu Israeli, na utakuwa mkuu wa watu wangu Israeli.’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Napo hapo kale, Sauli alipokuwa mfalme bado, aliyewaongoza Waisiraeli kwenda na kurudi vitani ni wewe, naye Bwana Mungu wako alikuambia: Wewe utawachunga walio ukoo wangu wa Waisiraeli, nawe wewe utawatawala hao walio ukoo wangu wa Waisiraeli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Katika zamani za kale, hata hapo Sauli alipokuwa mfalme, wewe ndiwe uliyewatoa na kuwaingiza Israeli. Naye BWANA, Mungu wako, akakuambia, Ndiwe, utakayewalisha watu wangu Israeli, ndiwe utakayekuwa mkuu juu ya watu wangu Israeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Zamani, Saulo alipokuwa mufalme wewe ndiwe uliyewaongoza Waisraeli katika vita, na Yawe, Mungu wako alikuambia: ‘Utakuwa muchungaji wa watu wangu Waisraeli, na utakuwa mukubwa wa watu wangu Waisraeli.’ ”