1 Chronicles 11:22 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye Benaya, mwana wa Yehoyada, kutoka Kabzeeli, alikuwa askari shujaa ambaye alifanya mambo mengi ya ajabu. Aliwaua mashujaa wawili kutoka Moabu, na siku moja wakati wa barafu, alishuka na kuua simba shimoni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Benaya mwana wa Yehoyada alikuwa mpiganaji hodari kutoka Kabseeli ambaye alifanya mambo makubwa ya ujasiri. Aliwaua mashujaa wawili hodari kuliko wote wa Moabu. Pia alishuka shimoni kulipokuwa na theluji na kumuua simba.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena, Benaya, mwana wa Yehoyada, mtu hodari, wa Kabseeli, aliyekuwa amefanya mambo makuu, ndiye aliyewaua simba wakali wawili wa Moabu;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye Benaya, mwana wa Yehoyada, kutoka Kabzeeli, alikuwa askari shujaa ambaye alifanya mambo mengi ya ajabu. Aliwaua mashujaa wawili kutoka Moabu, na siku moja wakati wa barafu, alishuka na kuua simba shimoni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Benaya, mwana wa Yehoyada alikuwa mpiganaji hodari kutoka Kabseeli, aliyefanya mambo makubwa ya ujasiri. Aliwaua watu wawili mashujaa wa Moabu. Pia aliingia shimoni siku ya theluji na kumwua simba.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Benaya, mwana wa Yehoyada alikuwa mpiganaji hodari kutoka Kabseeli ambaye alifanya mambo makubwa ya ujasiri. Aliwaua mashujaa wawili waliokuwa hodari kuliko wote wa Moabu. Pia alishuka shimoni kulipokuwa na theluji na kumuua simba.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena, Benaya, mwana wa Yehoyada, mtu hodari, wa Kabseeli, aliyekuwa amefanya mambo makuu, ndiye aliyewaua simba wakali wawili wa Moabu; pia akashuka, akamwua simba katikati ya shimo wakati wa theluji.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye Benaya, mwana wa Yehoyada, kutoka Kabzeeli, alikuwa askari shujaa ambaye alifanya mambo mengi ya ajabu. Aliwaua mashujaa wawili kutoka Moabu, na siku moja wakati wa barafu, alishuka na kuua simba shimoni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Benaya, mwana wa Yoyada, mwana wa mtu mwenye nguvu, alifanya matendo makuu, nako kwao kulikuwa Kabuseli. Yeye aliwaua wana wawili wa Arieli wa Moabu, tena siku moja, theluji ilipokuwa imeanguka, akashuka shimoni, akaua simba mlemle.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena, Benaya, mwana wa Yehoyada, mtu hodari, wa Kabseeli, aliyekuwa amefanya mambo makuu, ndiye aliyewaua simba wakali wawili wa Moabu; pia akashuka, akamwua simba katikati ya shimo wakati wa theluji.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Benaya mwana wa Yehoyada, kutoka muji wa Kabuseli, alikuwa askari shujaa ambaye alifanya mambo mengi ya ajabu. Aliua mashujaa wawili kutoka Moabu, na siku moja wakati wa baridi kali, akashuka na kuua simba ndani ya shimo.