1 Chronicles 11:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, wazee wote wa Israeli wakamwendea mfalme huko Hebroni; naye Daudi akafanya agano nao mbele ya Mwenyezi-Mungu, halafu wakampaka Daudi mafuta awe mfalme wa Waisraeli kulingana na neno la Mwenyezi-Mungu lililotolewa kwa njia ya Samueli.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wazee wote wa Israeli walipokuwa wamewasili kwa Mfalme Daudi huko Hebroni, alifanya mapatano nao huko Hebroni mbele za Mwenyezi Mungu, nao wakampaka Daudi mafuta awe mfalme wa Israeli, sawasawa na neno la Mwenyezi Mungu aliloahidi kupitia kwa Samweli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi wazee wote wa Israeli wakamjia mfalme huko Hebroni; naye Daudi akafanya agano nao huko Hebroni mbele za Bwana; nao wakamtia Daudi mafuta, awe mfalme wa Israeli, sawasawa na neno la Bwana kwa mkono wa Samweli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, wazee wote wa Israeli wakamwendea mfalme huko Hebroni; naye Daudi akafanya agano nao mbele ya Mwenyezi-Mungu, halafu wakampaka Daudi mafuta awe mfalme wa Waisraeli kulingana na neno la Mwenyezi-Mungu lililotolewa kwa njia ya Samueli.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wazee wote wa Israeli walipokuwa wamewasili kwa Mfalme Daudi huko Hebroni, alifanya mapatano nao huko Hebroni mbele za BWANA, nao wakamtia Daudi mafuta awe mfalme wa Israeli, sawasawa na BWANA alivyoahidi kupitia kwa Samweli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wazee wote wa Israeli walipokuwa wamewasili kwa Mfalme Daudi huko Hebroni, alifanya mapatano nao huko Hebroni mbele za bwana, nao wakamtia Daudi mafuta awe mfalme wa Israeli, sawasawa na bwana alivyoahidi kupitia kwa Samweli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi wazee wote wa Israeli wakamjia mfalme huko Hebroni; naye Daudi akafanya agano nao huko Hebroni mbele za BWANA; nao wakamtia Daudi mafuta, awe mfalme wa Israeli, sawasawa na neno la BWANA kwa mkono wa Samweli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, wazee wote wa Israeli wakamwendea mfalme huko Hebroni; naye Daudi akafanya agano nao mbele ya Mwenyezi-Mungu, halafu wakampaka Daudi mafuta awe mfalme wa Waisraeli kulingana na neno la Mwenyezi-Mungu lililotolewa kwa njia ya Samueli.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wazee wote wa Waisiraeli wakamjia mfalme huko Heburoni, Dawidi akafanya agano nao huko Heburoni mbele ya Bwana, wakampaka Dawidi mafuta, awe mfalme wao Waisiraeli, kama Bwana alivyosema kinywani mwa Samweli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi wazee wote wa Israeli wakamjia mfalme huko Hebroni; naye Daudi akafanya agano nao huko Hebroni mbele za BWANA; nao wakamtia Daudi mafuta, awe mfalme wa Israeli, sawasawa na neno la BWANA kwa mkono wa Samweli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, wazee wote wa Waisraeli wakamwendea mufalme kule Hebroni; naye Daudi akafanya agano nao mbele ya Yawe, halafu wakamupakaa Daudi mafuta akuwe mufalme wa Waisraeli kulingana na neno la Yawe lililotolewa kwa njia ya Samweli.