1 Chronicles 12:15 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hawa ndio watu waliovuka mto Yordani mnamo mwezi wa kwanza, mto ulipokuwa umefurika pande zote na kuwatawanya watu mashariki na magharibi ya mto.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hao ndio walivuka Mto Yordani katika mwezi wa kwanza ukiwa umefurika hadi kwenye kingo zake zote, wakawatorosha watu wote walioishi kwenye mabonde, kuelekea mashariki na magharibi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hao ndio wale waliovuka Yordani katika mwezi wa kwanza, ulipofurika kingo zake zote; nao wakawakimbiza wote wa bondeni kuelekea mashariki na magharibi pia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hawa ndio watu waliovuka mto Yordani mnamo mwezi wa kwanza, mto ulipokuwa umefurika pande zote na kuwatawanya watu mashariki na magharibi ya mto.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wao ndio walivuka Mto Yordani katika mwezi wa kwanza ukiwa umefurika hadi kwenye kingo zake zote na kusababisha watu wote waliokuwa wanaishi kwenye mabonde kukimbilia mashariki na wengine magharibi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wao ndio walivuka Mto Yordani katika mwezi wa kwanza ukiwa umefurika hadi kwenye kingo zake zote na kusababisha watu wote waliokuwa wanaishi kwenye mabonde kukimbilia mashariki na wengine magharibi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hao ndio wale waliovuka Yordani katika mwezi wa kwanza, ulipofurika kingo zake zote; nao wakawakimbiza wote wa bondeni kuelekea mashariki na magharibi pia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hawa ndio watu waliovuka mto Yordani mnamo mwezi wa kwanza, mto ulipokuwa umefurika pande zote na kuwatawanya watu mashariki na magharibi ya mto.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hawa ndio waliovuka Yordani katika mwezi wa kwanza, mto ulipojaa na kuzifurikia kingo zake zote mbili, wakawafukuza wote waliokaa huko mabondeni upande wa maawioni kwa jua na machweoni kwa jua.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hao ndio wale waliovuka Yordani katika mwezi wa kwanza, ulipofurika kingo zake zote; nao wakawakimbiza wote wa bondeni kuelekea mashariki na magharibi pia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hao watu wa kabila la Gadi walikuwa wakubwa wa waaskari. Kulingana na vyeo vyao, mudogo alisimamia kundi la waaskari mia moja, na mukubwa alisimamia kundi la waaskari elfu moja.