1 Chronicles 12:19 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Askari wengine wa kabila la Manase, walitoroka na kujiunga na Daudi, wakati alipoondoka pamoja na Wafilisti kwenda kupigana na mfalme Shauli. (Lakini hata hivyo, hakuwasaidia maana watawala wa Wafilisti walifanya shauri wamfukuze arudi Siklagi wakisema, “Tutayahatarisha maisha yetu kwa sababu atatutoroka arudi kwa bwana wake Shauli.”)
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baadhi ya watu kutoka kabila la Manase wakajiunga na Daudi alipoenda pamoja na Wafilisti kupigana na Sauli. (Daudi na watu wake hawakuwasaidia Wafilisti kwa sababu baada ya ushauri, watawala wao walimrudisha. Wakasema, “Itatugharimu vichwa vyetu kama Daudi atatuasi na kurudi kwa Sauli bwana wake.”)
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wa Manase pia wengine walimwangukia Daudi, alipokwenda pamoja na Wafilisti juu ya Sauli vitani, lakini hawakuwasaidia; kwani wale mabwana wa Wafilisti wakafanya shauri, wakamfukuza, wakisema, kwa hatari ya vichwa vyetu atamwangukia bwana wake Sauli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Askari wengine wa kabila la Manase, walitoroka na kujiunga na Daudi, wakati alipoondoka pamoja na Wafilisti kwenda kupigana na mfalme Shauli. (Lakini hata hivyo, hakuwasaidia maana watawala wa Wafilisti walifanya shauri wamfukuze arudi Siklagi wakisema, “Tutayahatarisha maisha yetu kwa sababu atatutoroka arudi kwa bwana wake Shauli.”)
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baadhi ya watu kutoka kabila la Manase wakajiunga na Daudi wakati alipokwenda pamoja na Wafilisti, kupigana na Sauli. (Daudi na watu wake hawakuwasaidia Wafilisti kwa sababu, baada ya ushauri, watawala wao walimrudisha. Wakasema, “Itatugharimu vichwa vyetu kama Daudi atatuasi na kurudi kwa Sauli bwana wake.”)
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baadhi ya watu kutoka kabila la Manase wakajiunga na Daudi wakati alikwenda pamoja na Wafilisti, kupigana na Sauli. (Daudi na watu wake hawakuwasaidia Wafilisti kwa sababu, baada ya ushauri, watawala wao walimrudisha. Wakasema, “Itatugharimu vichwa vyetu kama Daudi atatuasi na kurudi kwa Sauli bwana wake.”)
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Baadhi ya wana wa Manase walimwangukia Daudi, alipokwenda pamoja na Wafilisti juu ya Sauli vitani, lakini hawakuwasaidia; kwani wale mabwana wa Wafilisti wakafanya shauri, wakamfukuza, wakisema, tunahatarisha maisha yetu maana atamwangukia bwana wake Sauli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Askari wengine wa kabila la Manase, walitoroka na kujiunga na Daudi, wakati alipoondoka pamoja na Wafilisti kwenda kupigana na mfalme Shauli. (Lakini hata hivyo, hakuwasaidia maana watawala wa Wafilisti walifanya shauri wamfukuze arudi Siklagi wakisema, “Tutayahatarisha maisha yetu kwa sababu atatutoroka arudi kwa bwana wake Shauli.”)
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hata kwa Wamanase walikuwako waliourudia upande wa Dawidi, alipomjia Sauli pamoja na Wafilisti kupigana naye, lakini hawakuwasaidia; kwani wakuu wa Wafilisti walikuwa wamefanya shauri, kwa hiyo walikuwa wamempa ruhusa kwa kumwazia kwamba: Atarudi kwa bwana wake Sauli na kumtolea vichwa vyetu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wa Manase pia wengine walimwangukia Daudi, alipokwenda pamoja na Wafilisti juu ya Sauli vitani, lakini hawakuwasaidia; kwani wale mabwana wa Wafilisti wakafanya shauri, wakamfukuza, wakisema, kwa hatari ya vichwa vyetu atamwangukia bwana wake Sauli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu Roho akamujaza Amasai, mukubwa wa wale watu makumi tatu, naye akasema: “Sisi ni watu wako, ee Daudi! Tuko upande wako, ee mwana wa Yese! Amani, amani ikuwe kwako, na amani ikuwe kwa yeyote anayekusaidia! Maana Mungu wako ndiye anayekusaidia.” Kisha Daudi akawapokea na kuwafanya wakubwa katika kundi lake.