1 Chronicles 12:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hao walikuwa watu wa kabila la Benyamini kama alivyokuwa Shauli. Walikuwa wapiga upinde hodari, na warusha mawe kwa kombeo kwa kutumia mikono yote, wa kulia na kushoto.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Walikuwa na pinde na walikuwa na uwezo wa kupiga mishale au kutupa mawe kwa kombeo wakitumia mkono wa kushoto au wa kulia. Hawa walikuwa ndugu zake Sauli kutoka kabila la Benyamini):
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Walikuwa wenye kupinda upinde, nao walikuwa hodari wa kutumia mkono wa kuume na wa kushoto, kwa kutupa mawe ya teo, na kwa kupiga mishale ya upinde; walikuwa wa nduguze Sauli, wa Benyamini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hao walikuwa watu wa kabila la Benyamini kama alivyokuwa Shauli. Walikuwa wapiga upinde hodari, na warusha mawe kwa kombeo kwa kutumia mikono yote, wa kulia na kushoto.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
walikuwa na pinde na walikuwa na uwezo wa kupiga mishale au kutupa mawe kwa kombeo wakitumia mkono wa kushoto au wa kulia: hawa walikuwa ndugu zake Sauli kutoka kabila la Benyamini):
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
walikuwa na pinde na walikuwa na uwezo wa kupiga mishale au kutupa mawe kwa kombeo wakitumia mkono wa kushoto au wa kulia; hawa walikuwa ndugu zake Sauli kutoka kabila la Benyamini):
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Walikuwa wenye kupinda upinde, nao walikuwa hodari wa kutumia mkono wa kulia na wa kushoto, kwa kutupa mawe ya teo, na kwa kupiga mishale ya upinde; walikuwa wa nduguze Sauli, wa Benyamini.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hao walikuwa watu wa kabila la Benyamini kama alivyokuwa Shauli. Walikuwa wapiga upinde hodari, na warusha mawe kwa kombeo kwa kutumia mikono yote, wa kulia na kushoto.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Walishika pindi, nao walijua kutupa mawe kuumeni na kushotoni na kupiga mishale kwa pindi zao; nao walikuwa ndugu zake Sauli, maana ni Wabenyamini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Walikuwa wenye kupinda upinde, nao walikuwa hodari wa kutumia mkono wa kuume na wa kushoto, kwa kutupa mawe ya teo, na kwa kupiga mishale ya upinde; walikuwa wa nduguze Sauli, wa Benyamini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walikuwa wa kabila la Benjamina kama vile Saulo alivyokuwa. Walikuwa wapiga upinde hodari, na warusha mawe hodari kwa kutumia mikono yote, wa kuume na wa kushoto. Haya ndiyo majina yao: