1 Chronicles 12:20 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Daudi alipokuwa Siklagi, watu wafuatao wa kabila la Manase walimwendea: Adna, Yozabadi, Yediaeli, Mikaeli, Yozabadi, Elihu na Silethai. Kila mmoja wao alikuwa kiongozi wa kikosi cha watu 1,000 katika kabila la Manase.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Daudi alipoenda Siklagi, hawa ndio wanaume wa kabila la Manase waliojiunga naye: Adna, Yozabadi, Yediaeli, Mikaeli, Yozabadi, Elihu na Silethai, viongozi wa vikosi vya watu elfu moja katika kabila la Manase.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye alipokuwa akienda Siklagi, wakamwangukia hawa wa Manase, Adna, na Yozabadi, na Yediaeli, na Mikaeli, na Yozabadi, na Elihu, na Silethai, maakida wa maelfu waliokuwa wa Manase.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Daudi alipokuwa Siklagi, watu wafuatao wa kabila la Manase walimwendea: Adna, Yozabadi, Yediaeli, Mikaeli, Yozabadi, Elihu na Silethai. Kila mmoja wao alikuwa kiongozi wa kikosi cha watu 1,000 katika kabila la Manase.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Daudi alipokwenda Siklagi, hawa ndio watu wa kabila la Manase waliojiunga naye: Adna, Yozabadi, Yediaeli, Mikaeli, Yozabadi, Elihu na Silethai, viongozi wa vikosi vya watu 1,000 katika kabila la Manase.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Daudi alipokwenda Siklagi, hawa ndio watu wa kabila la Manase waliojiunga naye: Adna, Yozabadi, Yediaeli, Mikaeli, Yozabadi, Elihu na Silethai, viongozi wa vikosi vya watu 1,000 katika kabila la Manase.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye alipokuwa akienda Siklagi, Manase hawa wakamwangukia, Adna, na Yozabadi, na Yediaeli, na Mikaeli, na Yozabadi, na Elihu, na Silethai, makamanda wa maelfu waliokuwa wa Manase.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Daudi alipokuwa Siklagi, watu wafuatao wa kabila la Manase walimwendea: Adna, Yozabadi, Yediaeli, Mikaeli, Yozabadi, Elihu na Silethai. Kila mmoja wao alikuwa kiongozi wa kikosi cha watu 1,000 katika kabila la Manase.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha alipokwenda Siklagi, Wamanase hawa wakarudi upande wake: Adina na Yozabadi na Yediaeli na Mikaeli na Yozabadi na Elihu na Siltai, ndio wakuu wa vikosi vyenye watu elfu kwao Wamanase.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye alipokuwa akienda Siklagi, wakamwangukia hawa wa Manase, Adna, na Yozabadi, na Yediaeli, na Mikaeli, na Yozabadi, na Elihu, na Silethai, maakida wa maelfu waliokuwa wa Manase.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Waaskari wengine wa kabila la Manase, wakatoroka na kwenda kujiunga na Daudi, wakati alipoondoka pamoja na Wafilistini kwenda kupigana na mufalme Saulo. (Lakini hata hivyo, hakuwasaidia maana watawala wa Wafilistini walifanya shauri wamufukuze arudie Ziklagi wakisema: “Tutahatarisa maisha yetu kwa sababu atatutoroka na kurudia kwa bwana wake Saulo.”)