1 Chronicles 12:22 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku hata siku, watu walijiunga na Daudi kumsaidia, hatimaye akawa na jeshi kubwa sana, kama jeshi la Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Siku baada ya siku watu walikuja kumsaidia Daudi, hadi akawa na jeshi kubwa, kama jeshi la Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana siku kwa siku humjia Daudi watu wa kumsaidia, hata wakapata kuwa jeshi kubwa, kama jeshi la Mungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku hata siku, watu walijiunga na Daudi kumsaidia, hatimaye akawa na jeshi kubwa sana, kama jeshi la Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Siku baada ya siku watu walikuja kumsaidia Daudi, mpaka akawa na jeshi kubwa, kama jeshi la Mungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Siku baada ya siku watu walikuja kumsaidia Daudi, mpaka akawa na jeshi kubwa, kama jeshi la Mungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana siku baada ya siku watu waliomwendea Daudi ili kumsaidia, hadi wakapata kuwa jeshi kubwa, kama jeshi la Mungu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku hata siku, watu walijiunga na Daudi kumsaidia, hatimaye akawa na jeshi kubwa sana, kama jeshi la Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani siku hizo watu wakaja kwa Dawidi siku kwa siku, wamsaidie, mpaka wakiwa jeshi kubwa kama jeshi la Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana siku kwa siku humjia Daudi watu wa kumsaidia, hata wakapata kuwa jeshi kubwa, kama jeshi la Mungu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakamusaidia Daudi kupigana na makundi ya washambulizi, maana wote walikuwa waaskari mashujaa na majemadari wa waaskari.