1 Chronicles 12:39 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, walikaa na Daudi kwa muda wa siku tatu, wakila na kunywa kwani ndugu zao walikuwa wamekwisha waandalia vyakula.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watu hawa wakakaa huko na Daudi siku tatu, wakila na kunywa, kwa sababu jamaa zao zilikuwa zimewapatia mahitaji yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao walikuwako huko pamoja na Daudi siku tatu, wakila na kunywa; kwani ndugu zao walikuwa wamewaandalia tayari.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, walikaa na Daudi kwa muda wa siku tatu, wakila na kunywa kwani ndugu zao walikuwa wamekwisha waandalia vyakula.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watu hawa wakakaa huko na Daudi siku tatu, wakila na kunywa, kwa sababu jamaa zao zilikuwa zimewapatia mahitaji yao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watu hawa wakakaa huko na Daudi siku tatu, wakila na kunywa, kwa sababu jamaa zao zilikuwa zimewapatia mahitaji yao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao walikuwako huko pamoja na Daudi siku tatu, wakila na kunywa; kwani ndugu zao walikuwa wamewaandalia tayari.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, walikaa na Daudi kwa muda wa siku tatu, wakila na kunywa kwani ndugu zao walikuwa wamekwisha waandalia vyakula.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakawa huko pamoja na Dawidi wakila, wakinywa siku tatu, kwani ndugu zao waliwaandalia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao walikuwako huko pamoja na Daudi siku tatu, wakila na kunywa; kwani ndugu zao walikuwa wamewaandalia tayari.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Waaskari hao wote, waliojitayarisha kabisa kwa vita, walikwenda Hebroni na nia yao kubwa ikiwa ni kumuweka Daudi kuwa mufalme wa inchi yote ya Israeli. Nao watu wote wa Israeli, wakaungana wakiwa na nia moja ya kumuweka Daudi kuwa mufalme.