1 Chronicles 13:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mara Mwenyezi-Mungu akamkasirikia Uza kwa kulishika sanduku, akamuua. Uza akafa papo hapo mbele ya Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hasira ya Mwenyezi Mungu ikawaka dhidi ya Uza, akampiga kwa sababu aliuweka mkono wake kwenye Sanduku. Kwa hiyo akafa pale mbele za Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo hasira ya Bwana ikawaka juu ya Uza, naye akampiga, kwa sababu alilinyoshea sanduku mkono wake, hata akafa pale pale mbele za Mungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mara Mwenyezi-Mungu akamkasirikia Uza kwa kulishika sanduku, akamuua. Uza akafa papo hapo mbele ya Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hasira ya BWANA ikawaka dhidi ya Uza, akampiga kwa sababu aliuweka mkono wake kwenye Sanduku. Kwa hiyo akafa pale mbele za Mungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hasira ya bwana ikawaka dhidi ya Uza, akampiga kwa sababu aliuweka mkono wake kwenye Sanduku. Kwa hiyo akafa pale mbele za Mungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo hasira ya BWANA ikawaka juu ya Uza, naye akampiga, kwa sababu alilinyoshea sanduku mkono wake, hadi akafa pale pale mbele za Mungu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mara Mwenyezi-Mungu akamkasirikia Uza kwa kulishika sanduku, akamuua. Uza akafa papo hapo mbele ya Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, makali ya Bwana yalipomwakia Uza, akampiga, kwa kuwa amelipelekea hilo Sanduku mkono wake, akafa papo hapo mbele ya Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo hasira ya BWANA ikawaka juu ya Uza, naye akampiga, kwa sababu alilinyoshea sanduku mkono wake, hata akafa pale pale mbele za Mungu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mara moja Yawe akamukasirikia Uza kwa kuligusa sanduku, akamwua. Uza akakufa palepale mbele ya Mungu.