1 Chronicles 13:2 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha akawaambia Waisraeli wote waliokusanyika, “Ikiwa mtakubaliana nami, na ikiwa ni mapenzi yake Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, na tufanye hivi: Tutume wajumbe waende wakawaite ndugu zetu waliobaki nchini Israeli, pamoja na makuhani na Walawi walioko katika miji yao na malisho yao, waje wajumuike pamoja nasi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Daudi akawaambia kusanyiko lote la Israeli, “Mkiona ni vyema, na kama ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, tupeleke ujumbe kwa ndugu zetu wengine walio mbali na walio karibu katika nchi yote ya Israeli, pia kwa makuhani na Walawi walio pamoja nao katika miji yao na maeneo ya malisho ya miji hiyo, waje waungane na sisi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Daudi akawaambia jamii yote ya Israeli, Likiwa jema kwenu, tena likiwa limetoka kwa Bwana, Mungu wetu, na tutume watu huku na huku mahali pote kwa ndugu zetu waliosalia katika nchi yote ya Israeli, ambao pamoja nao makuhani na Walawi wamo ndani ya miji yao yenye viunga, ili wakusanyike kwetu;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha akawaambia Waisraeli wote waliokusanyika, “Ikiwa mtakubaliana nami, na ikiwa ni mapenzi yake Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, na tufanye hivi: tutume wajumbe waende wakawaite ndugu zetu waliobaki nchini Israeli, pamoja na makuhani na Walawi walioko katika miji yao na malisho yao, waje wajumuike pamoja nasi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo akaliambia kusanyiko lote la Israeli, “Kama mkiona ni vyema na kama ni mapenzi ya BWANA Mungu wetu, tupeleke ujumbe kwa ndugu zetu wengine walio mbali na walio karibu katika nchi yote ya Israeli, pia kwa makuhani na Walawi walio pamoja nao katika miji yao na katika sehemu zao za malisho yao waje waungane na sisi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Daudi akaliambia kusanyiko lote la Israeli, “Kama mkiona ni vyema, na kama ni mapenzi ya bwana Mwenyezi Mungu wetu, tupeleke ujumbe kwa ndugu zetu wengine walio mbali na walio karibu katika nchi yote ya Israeli, pia kwa makuhani na Walawi walio pamoja nao katika miji yao na katika sehemu zao za malisho yao, waje waungane na sisi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Daudi akawaambia jamii yote ya Israeli, Likiwa jema kwenu, tena likiwa limetoka kwa BWANA, Mungu wetu, na tutume watu huku na huku mahali pote kwa ndugu zetu waliosalia katika nchi yote ya Israeli, ambao pamoja nao makuhani na Walawi wamo ndani ya miji yao yenye viunga, ili wakusanyike kwetu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha akawaambia Waisraeli wote waliokusanyika, “Ikiwa mtakubaliana nami, na ikiwa ni mapenzi yake Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, na tufanye hivi: Tutume wajumbe waende wakawaite ndugu zetu waliobaki nchini Israeli, pamoja na makuhani na Walawi walioko katika miji yao na malisho yao, waje wajumuike pamoja nasi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
kisha Dawidi akauambia mkutano wote wa Waisiraeli: Mkiona kuwa vema, tena vikiwa vimetoka kwake Bwana Mungu wetu, na tutume pande zote po pote kwa ndugu zetu waliosalia katika nchi zote za Isiraeli, hata kwa watambikaji na kwa Walawi katika miji yao, wanamokaa, kuwaambia, wakusanyike kwetu,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Daudi akawaambia jamii yote ya Israeli, Likiwa jema kwenu, tena likiwa limetoka kwa BWANA, Mungu wetu, na tutume watu huku na huku mahali pote kwa ndugu zetu waliosalia katika nchi yote ya Israeli, ambao pamoja nao makuhani na Walawi wamo ndani ya miji yao yenye viunga, ili wakusanyike kwetu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha akawaambia Waisraeli wote waliokusanyika: “Ikiwa mutakubaliana nami, na ikiwa ni mapenzi ya Yawe, Mungu wetu, tufanye hivi: tutume wajumbe waende wawaite wandugu zetu waliobaki katika inchi ya Israeli, pamoja na makuhani na Walawi wanaokuwa katika miji yao na mashamba ya malisho yao, wakuje kukusanyika pamoja nasi.