1 Chronicles 13:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hivyo, Daudi aliwakusanya Waisraeli wote nchini; toka kijito cha Shihori kilichoko Misri, hadi maingilio ya Hamathi ili kulileta sanduku la Mungu toka Kiriath-yearimu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi Daudi akawakusanya Waisraeli wote, kuanzia Mto Shihori ulioko Misri hadi Lebo-Hamathi, ili kulileta Sanduku la Mungu kutoka Kiriath-Yearimu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Daudi akawakusanya Israeli wote, toka Shihori, kijito cha Misri, hata pa kuingilia Hamathi, ili kwamba walilete sanduku la Mungu kutoka Kiriath-yearimu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hivyo, Daudi aliwakusanya Waisraeli wote nchini; toka kijito cha Shihori kilichoko Misri, hadi maingilio ya Hamathi ili kulileta sanduku la Mungu toka Kiriath-yearimu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi Daudi akawakusanya Waisraeli wote, kuanzia Mto Shihori ulioko Misri hadi Lebo-Hamathi, ili kulileta Sanduku la Mungu kutoka Kiriath-Yearimu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi Daudi akawakusanya Waisraeli wote, kuanzia Mto Shihori ulioko Misri hadi Lebo-Hamathi, ili kulileta Sanduku la Mungu kutoka Kiriath-Yearimu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Daudi akawakusanya Israeli wote, toka Shihori, kijito cha Misri, hadi pa kuingilia Hamathi, ili walilete sanduku la Mungu kutoka Kiriath-yearimu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hivyo, Daudi aliwakusanya Waisraeli wote nchini; toka kijito cha Shihori kilichoko Misri, hadi maingilio ya Hamathi ili kulileta sanduku la Mungu toka Kiriath-yearimu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo Dawidi akawakusanya Waisiraeli wote toka Sihori katika Misri hata kufika Hamati, waje kulichukua Sanduku la Mungu huko Kiriati-Yearimu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Daudi akawakusanya Israeli wote, toka Shihori, kijito cha Misri, hata pa kuingilia Hamathi, ili kwamba walilete sanduku la Mungu kutoka Kiriath-yearimu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo, Daudi akawakusanya Waisraeli wote katika inchi, tokea kwenye kijito cha Sihori kinachokuwa Misri, mpaka kwenye kiingilio cha Hamati kwa kulileta Sanduku la Agano toka Kiriati-Yearimu.