1 Chronicles 13:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Daudi, akiandamana na Waisraeli wote, akaenda hadi mjini Baala, yaani Kiriath-yearimu, nchini Yudea, ili kulichukua toka huko sanduku la Mungu linaloitwa kwa jina lake Mwenyezi-Mungu akaaye kwenye kiti chake cha enzi juu ya viumbe vyenye mabawa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Daudi akiwa pamoja na Waisraeli wote wakaenda Baala ya Yuda (yaani Kiriath-Yearimu) kulipandisha Sanduku la Mungu Mwenyezi Mungu, yeye anayeketi kwenye kiti cha enzi kati ya makerubi: Sanduku linaloitwa kwa Jina lake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Daudi akapanda, yeye na Israeli wote, mpaka Baala, ndio Kiriath-yearimu, ulio wa Yuda, ili kulileta toka huko sanduku la Mungu, Bwana akaaye juu ya makerubi, lililoitwa kwa Jina lake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Daudi, akiandamana na Waisraeli wote, akaenda hadi mjini Baala, yaani Kiriath-yearimu, nchini Yudea, ili kulichukua toka huko sanduku la Mungu linaloitwa kwa jina lake Mwenyezi-Mungu akaaye kwenye kiti chake cha enzi juu ya viumbe vyenye mabawa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Daudi akiwa pamoja na Waisraeli wote wakaenda Baada ya Yuda (Kiriath-Yearimu) kulipandisha Sanduku la Mungu BWANA kutoka huko, ambaye anaketi katika kiti chake cha enzi kilichoko kati ya makerubi, sanduku ambalo linaitwa kwa Jina lake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Daudi akiwa pamoja na Waisraeli wote wakaenda Baala ya Yuda (yaani Kiriath-Yearimu) kulipandisha Sanduku la Mungu bwana, yeye anayeketi katika kiti cha enzi kati ya makerubi: Sanduku linaloitwa kwa Jina lake, kutoka huko.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Daudi akapanda, yeye na Israeli wote, mpaka Baala, ndio Kiriath-yearimu, ulio wa Yuda, ili kulileta toka huko sanduku la Mungu, BWANA akaaye juu ya makerubi, lililoitwa kwa Jina lake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Daudi, akiandamana na Waisraeli wote, akaenda hadi mjini Baala, yaani Kiriath-yearimu, nchini Yudea, ili kulichukua toka huko sanduku la Mungu linaloitwa kwa jina lake Mwenyezi-Mungu akaaye kwenye kiti chake cha enzi juu ya viumbe vyenye mabawa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Dawidi na Waisiraeli wote wakapanda kwenda Bala, ndio Kiriati-Yearimu ulio mji wa Yuda, kulichukua huko Sanduku la Mungu Bwana akaaye juu ya Makerubi, kwa maana hili liliitwa kwa Jina lake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Daudi akapanda, yeye na Israeli wote, mpaka Baala, ndio Kiriath-yearimu, ulio wa Yuda, ili kulileta toka huko sanduku la Mungu, BWANA akaaye juu ya makerubi, lililoitwa kwa Jina lake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Daudi akiandamana na Waisraeli wote, akaenda mpaka katika muji wa Bala, ni kusema Kiriati-Yearimu, katika inchi ya Yudea, kwa kulitwaa toka kule Sanduku la Agano linaloitwa kwa jina la Yawe anayeikaa kwenye kiti chake cha kifalme juu ya makerubi.