1 Chronicles 13:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Daudi na Waisraeli wote wakawa wanacheza kwa nguvu zao zote, mbele ya Mungu. Waliimba huku wanapiga ala za muziki zilizotengenezwa kwa mvinje: Vinubi, vinanda, matari, matoazi na tarumbeta.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Daudi pamoja na Waisraeli wote walikuwa wanasifu kwa nguvu zao zote mbele za Mungu, kwa nyimbo na kwa vinubi, zeze, matari, matoazi na tarumbeta.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakacheza Daudi na Israeli wote, mbele za Mungu, kwa nguvu zao zote; na kwa nyimbo na kwa vinubi, na kwa vinanda, na kwa matari, na kwa matoazi, na kwa tarumbeta.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Daudi na Waisraeli wote wakawa wanacheza kwa nguvu zao zote, mbele ya Mungu. Waliimba huku wanapiga ala za muziki zilizotengenezwa kwa mvinje: vinubi, vinanda, matari, matoazi na tarumbeta.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Daudi pamoja na Waisraeli wote walikuwa wanasifu kwa nguvu zao zote mbele za Mungu, kwa nyimbo na kwa vinubi, zeze, matari, matoazi na tarumbeta.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Daudi pamoja na Waisraeli wote walikuwa wanasifu kwa nguvu zao zote mbele za Mungu, kwa nyimbo na kwa vinubi, zeze, matari, matoazi na tarumbeta.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakacheza Daudi na Israeli wote, mbele za Mungu, kwa nguvu zao zote; na kwa nyimbo na kwa vinubi, na kwa vinanda, na kwa matari, na kwa matoazi, na kwa tarumbeta.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Daudi na Waisraeli wote wakawa wanacheza kwa nguvu zao zote, mbele ya Mungu. Waliimba huku wanapiga ala za muziki zilizotengenezwa kwa mvinje: Vinubi, vinanda, matari, matoazi na tarumbeta.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Dawidi mwenyewe na Waisiraeli wote wakalitangulia na kucheza mbele ya Mungu kwa nguvu zote na kumwimbia pamoja na kupiga mazeze na mapango na patu na matoazi na matarumbeta.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakacheza Daudi na Israeli wote, mbele za Mungu, kwa nguvu zao zote; na kwa nyimbo na kwa vinubi, na kwa vinanda, na kwa matari, na kwa matoazi, na kwa tarumbeta.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Daudi na Waisraeli wote wakakuwa wanacheza kwa nguvu zao zote, mbele ya Mungu. Waliimba nao wakikuwa wanapiga ala za muziki zilizotengenezwa kwa muti wa muvinje: vinubi, vinanda, matari, matoazi na baragumu.