1 Chronicles 14:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Daudi akaenda huko Baal-perasimu, akawashinda; halafu akasema, “Mungu amepita katikati ya adui zangu kwa mkono wangu, kama mafuriko ya maji yaendayo kasi.” Kwa hiyo mahali hapo panaitwa Baal-perasimu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo Daudi pamoja na watu wake wakakwea hadi Baal-Perasimu, akawashinda huko. Akasema, “Kama maji yanavyofurika, Mungu amewafurikia adui zangu kwa kutumia mkono wangu.” Kwa hiyo mahali pale pakaitwa Baal-Perasimu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi wakapanda mpaka Baal-perasimu, Daudi naye akawapiga huko; Daudi akasema, Bwana amewafurikia adui zangu kwa mkono wangu, kama mafuriko ya maji. Basi wakapaita mahali pale jina lake Baal-perasimu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Daudi akaenda huko Baal-perasimu, akawashinda; halafu akasema, “Mungu amepita katikati ya adui zangu kwa mkono wangu, kama mafuriko ya maji yaendayo kasi.” Kwa hiyo mahali hapo panaitwa Baal-perasimu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo Daudi pamoja na watu wake wakakwea mpaka Baal-Perasimu, akawashinda huko. Akasema, “Kama maji yafurikayo, Mungu amewafurikia adui zangu kwa kutumia mkono wangu.” Kwa hiyo mahali pale pakaitwa Baal-Perasimu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo Daudi pamoja na watu wake wakakwea mpaka Baal-Perasimu, akawashinda huko. Akasema, “Kama maji yafurikavyo, Mungu amewafurikia adui zangu kwa kutumia mkono wangu.” Kwa hiyo mahali pale pakaitwa Baal-Perasimu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi wakapanda mpaka Baal-perasimu, Daudi naye akawapiga huko; Daudi akasema, BWANA amewafurikia adui zangu kwa mkono wangu, kama mafuriko ya maji. Basi wakapaita mahali pale jina lake Baal-perasimu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Daudi akaenda huko Baal-perasimu, akawashinda; halafu akasema, “Mungu amepita katikati ya adui zangu kwa mkono wangu, kama mafuriko ya maji yaendayo kasi.” Kwa hiyo mahali hapo panaitwa Baal-perasimu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, walipopanda Baali-Perasimu; Dawidi alipowapiga huko, akasema yeye Dawidi: Mungu amewaatua adui zangu kwa nguvu ya mkono wangu, kama maji yanavyoatua ukingo. Kwa sababu hii wakapaita mahali pale Baali-Perasimu (Maatuko).
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi wakapanda mpaka Baal-perasimu, Daudi naye akawapiga huko; Daudi akasema, BWANA amewafurikia adui zangu kwa mkono wangu, kama mafuriko ya maji. Basi wakapaita mahali pale jina lake Baal-perasimu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Daudi akaenda kule Bali-Perasimu, akawashinda; halafu akasema: “Mungu amebomoa ukingo wa waadui zangu kwa mukono wangu, kama mafuriko ya maji yanayoenda mbio.” Kwa hiyo pahali pale panaitwa “Bwana Mwenye Kubomoa.”