1 Chronicles 14:8 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wafilisti waliposikia kwamba Daudi amepakwa mafuta kuwa mfalme wa nchi nzima ya Israeli, wote walitoka kwa wingi kwenda kumtafuta. Daudi alipopata habari, alitoka kwenda kuwakabili.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wafilisti waliposikia kuwa Daudi amepakwa mafuta kuwa mfalme wa Israeli yote, wakapanda na jeshi lao lote kwenda kumsaka, lakini Daudi akapata habari hizo, naye akatoka ili kwenda kukabiliana nao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na waliposikia hao Wafilisti ya kwamba Daudi ametiwa mafuta ili awe mfalme juu ya Israeli wote, Wafilisti wote wakapanda kumtafuta Daudi; naye Daudi akasikia, akatoka nje kupigana nao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wafilisti waliposikia kwamba Daudi amepakwa mafuta kuwa mfalme wa nchi nzima ya Israeli, wote walitoka kwa wingi kwenda kumtafuta. Daudi alipopata habari, alitoka kwenda kuwakabili.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati Wafilisti waliposikia kwamba Daudi ametiwa mafuta kuwa mfalme katika Israeli yote, wakaondoka na jeshi lao lote ili kwenda kumsaka, lakini Daudi akapata habari naye akatoka ili kwenda kukabiliana nao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wafilisti waliposikia kuwa Daudi ametiwa mafuta kuwa mfalme wa Israeli yote, wakapanda na jeshi lao lote kwenda kumsaka, lakini Daudi akapata habari hizo, naye akatoka ili kwenda kukabiliana nao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wafilisti waliposikia ya kwamba Daudi ametiwa mafuta ili awe mfalme wa Israeli wote, Wafilisti wote wakapanda kumtafuta Daudi; naye Daudi akasikia, akatoka nje kupigana nao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wafilisti waliposikia kwamba Daudi amepakwa mafuta kuwa mfalme wa nchi nzima ya Israeli, wote walitoka kwa wingi kwenda kumtafuta. Daudi alipopata habari, alitoka kwenda kuwakabili.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wafilisti waliposikia, ya kuwa Dawidi amepakwa mafuta, awe mfalme wao Waisiraeli wote, ndipo, Wafilisti wote walipopanda kumtafuta Dawidi. Dawidi alipovisikia akatoka kukutana nao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na waliposikia hao Wafilisti ya kwamba Daudi ametiwa mafuta ili awe mfalme juu ya Israeli wote, Wafilisti wote wakapanda kumtafuta Daudi; naye Daudi akasikia, akatoka nje kupigana nao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wafilistini waliposikia kwamba Daudi amepakwa mafuta kuwa mufalme wa inchi nzima ya Waisraeli, wote wakatoka kwa wingi kwenda kumutafuta. Daudi alipopata habari, akatoka kwenda kupigana nao.