1 Chronicles 15:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
akawaambia, “Nyinyi ni viongozi wa koo za Walawi. Jitakaseni pamoja na ndugu zenu, ili mkalilete sanduku la Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, hadi mahali ambapo nimelitayarishia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akawaambia, “Ninyi ndio viongozi wa jamaa za Walawi. Ninyi pamoja na Walawi wenzenu inawapasa mjitakase na kulipandisha Sanduku la Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, hadi mahali pale nimetengeneza kwa ajili yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
akawaambia, Ninyi ni vichwa vya mbari za baba za Walawi; jitakaseni, ninyi na ndugu zenu, ili mlipandishe sanduku la Bwana, Mungu wa Israeli, mpaka mahali pale nilipoliwekea tayari.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
akawaambia, “Nyinyi ni viongozi wa koo za Walawi. Jitakaseni pamoja na ndugu zenu, ili mkalilete sanduku la Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, hadi mahali ambapo nimelitayarishia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
akawaambia, “Ninyi ndio viongozi wa jamaa za Walawi. Ninyi pamoja na Walawi wenzenu inawapasa mjitakase na kulipandisha Sanduku la BWANA, Mungu wa Israeli hadi mahali ambapo nimetengeneza kwa ajili yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akawaambia, “Ninyi ndio viongozi wa jamaa za Walawi. Ninyi pamoja na Walawi wenzenu inawapasa mjitakase na kulipandisha Sanduku la bwana, Mungu wa Israeli hadi mahali ambapo nimetengeneza kwa ajili yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
akawaambia, Ninyi ni vichwa vya koo za baba za Walawi; jitakaseni, ninyi na ndugu zenu, ili mlipandishe sanduku la BWANA, Mungu wa Israeli, mpaka mahali pale nilipolitayarishia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
akawaambia, “Nyinyi ni viongozi wa koo za Walawi. Jitakaseni pamoja na ndugu zenu, ili mkalilete sanduku la Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, hadi mahali ambapo nimelitayarishia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
akawaambia: Ninyi m wakuu wa milango ya Walawi, jitakaseni ninyi na ndugu zenu! Kisha mtalipandisha Sanduku la Bwana Mungu wa Isiraeli na kuliweka mahali pake, nilipolitengenezea.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
akawaambia, Ninyi ni vichwa vya mbari za baba za Walawi; jitakaseni, ninyi na ndugu zenu, ili mlipandishe sanduku la BWANA, Mungu wa Israeli, mpaka mahali pale nilipoliwekea tayari.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
akawaambia: “Ninyi ni viongozi wa ukoo za Walawi. Mujitakase pamoja na wandugu zenu, mupate kuleta Sanduku la Agano la Yawe, Mungu wa Israeli, mpaka pahali ambapo nimelitayarishia.