1 Chronicles 15:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa sababu hamkulibeba safari ya kwanza, Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, alituadhibu kwani hatukulitunza kama alivyoagiza.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ilikuwa ni kwa sababu hii, ninyi Walawi, hamkulipandisha Sanduku la Mwenyezi Mungu mara ya kwanza, hata ikasababisha Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, kuwaka hasira dhidi yetu. Hatukumuuliza jinsi ya kufanya ili tupate kulileta jinsi alivyoagiza.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwani kwa sababu ninyi hamkulichukua safari ya kwanza, Bwana, Mungu wetu, alitufurikia, kwa maana hatukumtafuta sawasawa na sheria.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa sababu hamkulibeba safari ya kwanza, Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, alituadhibu kwani hatukulitunza kama alivyoagiza.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ilikuwa ni kwa sababu hii, ninyi Walawi, hamkulipandisha Sanduku la BWANA mara ya kwanza, hata ikasababisha BWANA Mungu wetu kuwaka hasira dhidi yetu. Hatukumwuliza jinsi ya kufanya ili tupate kulileta jinsi alivyoagiza.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ilikuwa ni kwa sababu hii, ninyi Walawi, hamkulipandisha Sanduku la bwana mara ya kwanza, hata ikasababisha bwana Mwenyezi Mungu wetu kuwaka hasira dhidi yetu. Hatukumuuliza jinsi ya kufanya ili tupate kulileta jinsi alivyoagiza.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa kuwa ninyi hamkulichukua safari ya kwanza, BWANA, Mungu wetu, alitufurikia, kwa maana hatukumtafuta kulingana na sheria.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa sababu hamkulibeba safari ya kwanza, Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, alituadhibu kwani hatukulitunza kama alivyoagiza.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa kuwa mara ya kwanza hamkuwako. Bwana Mungu wetu akatupiga pigo, kwa kuwa hatukumtafuta kwa njia itupasayo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwani kwa sababu ninyi hamkulichukua safari ya kwanza, BWANA, Mungu wetu, alitufurikia, kwa maana hatukumtafuta sawasawa na sheria.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa sababu hamukulibeba safari ya kwanza, Yawe, Mungu wetu, akatuazibu maana hatukulitunza kama vile alivyoagiza.”