1 Chronicles 15:27 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Daudi alikuwa amevaa joho la kitani safi, hali kadhalika na Walawi wote waliobeba sanduku, waimbaji na Kenania kiongozi wa waimbaji. Mbali na joho hilo, Daudi alikuwa amevaa kizibao cha kitani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi Daudi alikuwa amevaa joho la kitani safi, kama walivyokuwa wamevaa Walawi wote waliokuwa wanalichukua lile Sanduku, waimbaji nao walivaa vivyo hivyo, pamoja na Kenania aliyekuwa anaongoza nyimbo za waimbaji. Daudi alivaa pia kizibau cha kitani safi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Daudi alikuwa amevaa joho ya kitani safi, na Walawi wote waliolichukua sanduku, na waimbaji, na Kenania msimamizi wa uchukuzi, na waimbaji; naye Daudi alikuwa amevaa naivera ya kitani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Daudi alikuwa amevaa joho la kitani safi, hali kadhalika na Walawi wote waliobeba sanduku, waimbaji na Kenania kiongozi wa waimbaji. Mbali na joho hilo, Daudi alikuwa amevaa kizibao cha kitani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi Daudi alikuwa amevaa joho la kitani safi, kama walivyokuwa wamevaa Walawi wote waliokuwa wanalichukua lile Sanduku, waimbaji nao walivaa vivyo hivyo, pamoja na Kenania aliyekuwa anaongoza nyimbo za waimbaji. Daudi alivaa pia kisibau cha kitani safi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi Daudi alikuwa amevaa joho la kitani safi, kama walivyokuwa wamevaa Walawi wote waliokuwa wanalichukua lile Sanduku, waimbaji nao walivaa vivyo hivyo, pamoja na Kenania aliyekuwa anaongoza nyimbo za waimbaji. Daudi alivaa pia kisibau cha kitani safi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Daudi alikuwa amevaa joho la kitani safi, na Walawi wote waliolichukua sanduku, na waimbaji, na Kenania msimamizi wa uchukuzi, na waimbaji; naye Daudi alikuwa amevaa naivera ya kitani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Daudi alikuwa amevaa joho la kitani safi, hali kadhalika na Walawi wote waliobeba sanduku, waimbaji na Kenania kiongozi wa waimbaji. Mbali na joho hilo, Daudi alikuwa amevaa kizibao cha kitani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Dawidi alikuwa amevaa kanzu ya bafta, hata Walawi wote waliolichukua hilo Sanduku na waimbaji na Kenania, mkuu wao waimbaji aliyewaimbisha, naye Dawidi alikuwa amevaa kisibau cheupe cha ukonge.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Daudi alikuwa amevaa joho ya kitani safi, na Walawi wote waliolichukua sanduku, na waimbaji, na Kenania msimamizi wa uchukuzi, na waimbaji; naye Daudi alikuwa amevaa naivera ya kitani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Daudi alikuwa akivaa kanzu ya kitani safi, hata vilevile na Walawi wote waliobeba sanduku, waimbaji na Kenania kiongozi wa waimbaji. Zaidi ya kanzu ile, Daudi alikuwa akivaa kizibao cha kitani.