1 Chronicles 15:28 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hivyo, Waisraeli wote walijumuika pamoja kwa shangwe kulichukua sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu hadi Yerusalemu. Walilisindikiza kwa mlio wa baragumu, tarumbeta, matoazi, na sauti kubwa za vinanda na vinubi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo Israeli wote wakalipandisha Sanduku la Agano la Mwenyezi Mungu kwa shangwe, wakipiga pembe za kondoo dume, tarumbeta, na kucheza matoazi, zeze na vinubi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndivyo Israeli wote walivyolipandisha sanduku la agano la Bwana kwa shangwe na kwa sauti ya tarumbeta, na kwa baragumu, na kwa matoazi, wakipiga sauti kuu kwa vinanda na vinubi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hivyo, Waisraeli wote walijumuika pamoja kwa shangwe kulichukua sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu hadi Yerusalemu. Walilisindikiza kwa mlio wa baragumu, tarumbeta, matoazi, na sauti kubwa za vinanda na vinubi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo Israeli wote wakalipandisha Sanduku la Agano la BWANA kwa shangwe, wakipiga pembe za kondoo waume, tarumbeta, matoazi, wakipiga zeze na vinubi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo Israeli wote wakalipandisha Sanduku la Agano la bwana kwa shangwe, wakipiga pembe za kondoo dume, tarumbeta, matoazi, wakipiga zeze na vinubi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndivyo Israeli wote walivyolipandisha sanduku la Agano la BWANA kwa shangwe na kwa sauti ya tarumbeta, na kwa baragumu, na kwa matoazi, wakipiga sauti kuu kwa vinanda na vinubi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hivyo, Waisraeli wote walijumuika pamoja kwa shangwe kulichukua sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu hadi Yerusalemu. Walilisindikiza kwa mlio wa baragumu, tarumbeta, matoazi, na sauti kubwa za vinanda na vinubi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao Waisiraeli wote wakalipandisha Sanduku la Agano la Bwana kwa kushangilia na kwa kupiga mabaragumu na matarumbeta na matoazi pamoja na kuyavumisha nayo mapango na mazeze.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndivyo Israeli wote walivyolipandisha sanduku la agano la BWANA kwa shangwe na kwa sauti ya tarumbeta, na kwa baragumu, na kwa matoazi, wakipiga sauti kuu kwa vinanda na vinubi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hivyo, Waisraeli wote wakakusanyika pamoja kwa shangwe kwa kubeba Sanduku la Agano la Yawe mpaka Yerusalema. Wakalisindikiza kwa mulio wa baragumu, ngunga, matoazi, na sauti kubwa za vinanda na vinubi.