1 Chronicles 15:29 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu lilipokuwa linaingia katika mji wa Daudi, Mikali, binti Shauli, alichungulia dirishani, akamwona mfalme Daudi akicheza na kushangilia, basi akamdharau moyoni mwake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sanduku la Agano la Mwenyezi Mungu lilipokuwa linaingia Mji wa Daudi, Mikali binti Sauli akachungulia dirishani. Naye alipomwona Mfalme Daudi akicheza na kusherehekea, akamdharau moyoni mwake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata ikawa, sanduku la agano la Bwana lilipofika mjini kwa Daudi, Mikali binti Sauli akachungulia dirishani, akamwona mfalme Daudi, akicheza na kushangilia; akamdharau moyoni mwake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu lilipokuwa linaingia katika mji wa Daudi, Mikali, binti Shauli, alichungulia dirishani, akamwona mfalme Daudi akicheza na kushangilia, basi akamdharau moyoni mwake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati Sanduku la Agano la BWANA lilipokuwa linaingia katika Mji wa Daudi, Mikali binti Sauli akachungulia dirishani. Alipomwona Mfalme Daudi akicheza na kusifu, akamdharau moyoni mwake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sanduku la Agano la bwana lilipokuwa linaingia katika Mji wa Daudi, Mikali binti Sauli akachungulia dirishani. Naye alipomwona Mfalme Daudi akicheza na kusherehekea, akamdharau moyoni mwake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata ikawa, sanduku la Agano la BWANA lilipofika mjini kwa Daudi, Mikali binti Sauli akachungulia dirishani, akamwona mfalme Daudi, akicheza na kushangilia; akamdharau moyoni mwake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu lilipokuwa linaingia katika mji wa Daudi, Mikali, binti Shauli, alichungulia dirishani, akamwona mfalme Daudi akicheza na kushangilia, basi akamdharau moyoni mwake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa, Sanduku la Agano la Bwana lilipoingia mjini kwa Dawidi, Mikali, binti Sauli, alichungulia dirishani, naye alipomwona mfalme Dawidi, jinsi alivyorukaruka na kuchezacheza, ndipo, alipombeza moyoni mwake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata ikawa, sanduku la agano la BWANA lilipofika mjini kwa Daudi, Mikali binti Sauli akachungulia dirishani, akamwona mfalme Daudi, akicheza na kushangilia; akamdharau moyoni mwake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sanduku la Agano la Yawe lilipokuwa likiingia katika muji wa Daudi, Mikali, binti wa Saulo, akachungulia kwenye dirisha, akamwona mufalme Daudi akicheza na kushangilia, basi akamuzarau ndani ya moyo wake.