1 Chronicles 16:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Zaidi ya hayo, Daudi aliwateua baadhi ya Walawi wawe wahudumu wa sanduku la Mwenyezi-Mungu, wamtukuze, wamtolee shukrani na wamsifu Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akawaweka pia baadhi ya Walawi ili wahudumu mbele ya Sanduku la Mwenyezi Mungu kufanya maombi, kumshukuru na kumsifu Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli:
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akawaagiza baadhi ya Walawi kwamba watumike mbele ya sanduku la Bwana, wamfanyie ukumbusho, na shukrani, na sifa, Bwana, Mungu wa Israeli;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Zaidi ya hayo, Daudi aliwateua baadhi ya Walawi wawe wahudumu wa sanduku la Mwenyezi-Mungu, wamtukuze, wamtolee shukrani na wamsifu Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akawaweka pia baadhi ya Walawi ili wahudumu mbele ya Sanduku la BWANA kufanya maombi, kumshukuru na kumsifu BWANA, Mungu wa Israeli:
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akawaweka pia baadhi ya Walawi ili wahudumu mbele ya Sanduku la bwana kufanya maombi, kumshukuru na kumsifu bwana, Mungu wa Israeli:
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akawaagiza baadhi ya Walawi kwamba watumike mbele ya sanduku la BWANA, wamfanyie ukumbusho, na shukrani, na sifa, BWANA, Mungu wa Israeli;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Zaidi ya hayo, Daudi aliwateua baadhi ya Walawi wawe wahudumu wa sanduku la Mwenyezi-Mungu, wamtukuze, wamtolee shukrani na wamsifu Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akaweka Walawi wengine, watumike hapo penye Sanduku la Bwana na kuwakumbusha watu, Bwana Mungu wa Isiraeli aliyoyafanya, wamshukuru na kumtukuza,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akawaagiza baadhi ya Walawi kwamba watumike mbele ya sanduku la BWANA, wamfanyie ukumbusho, na shukrani, na sifa, BWANA, Mungu wa Israeli;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Zaidi ya hayo, Daudi akaweka Walawi wamoja kwa kazi mbele ya Sanduku la Agano la Yawe, wamutukuze, wamutolee shukrani na wamusifu Yawe, Mungu wa Israeli.