1 Chronicles 16:41 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Pamoja nao walikuwa Hemani na Yeduthuni na wale wote waliochaguliwa, waliotajwa majina yao, ili kumshukuru Mwenyezi-Mungu kwa kuwa fadhili zake ni za milele.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Waliohudumu pamoja nao walikuwa Hemani, Yeduthuni na wale wote waliochaguliwa na kutajwa kwa jina kumpa Mwenyezi Mungu shukrani, “Kwa maana fadhili zake zadumu milele.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na pamoja nao Hemani na Yeduthuni, na wale wengine waliochaguliwa, waliotajwa majina yao, ili kumshukuru Bwana, kwa kuwa fadhili zake ni za milele;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Pamoja nao walikuwa Hemani na Yeduthuni na wale wote waliochaguliwa, waliotajwa majina yao, ili kumshukuru Mwenyezi-Mungu kwa kuwa fadhili zake ni za milele.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Waliohudumu pamoja nao walikuwa Hemani, Yeduthuni na wale wote waliochaguliwa na kutajwa kwa jina kumpa BWANA shukrani, “Kwa maana fadhili zake zadumu milele.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Waliohudumu pamoja nao walikuwa Hemani, Yeduthuni na wale wote waliochaguliwa na kutajwa kwa jina kumpa bwana shukrani, “Kwa maana fadhili zake zadumu milele.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na pamoja nao Hemani na Yeduthuni, na wale wengine waliochaguliwa, waliotajwa majina yao, ili kumshukuru BWANA, kwa kuwa fadhili zake ni za milele;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Pamoja nao walikuwa Hemani na Yeduthuni na wale wote waliochaguliwa, waliotajwa majina yao, ili kumshukuru Mwenyezi-Mungu kwa kuwa fadhili zake ni za milele.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Pamoja nao walikuwako Hemani na Yedutuni nao wengine wote waliochaguliwa na kuandikwa majina, waimbe: Mshukuruni Bwana, ya kuwa upole wake ni wakale na kale!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na pamoja nao Hemani na Yeduthuni, na wale wengine waliochaguliwa, waliotajwa majina yao, ili kumshukuru BWANA, kwa kuwa fadhili zake ni za milele;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Pamoja nao kulikuwa Hemani na Yedutuni na wale wote waliochaguliwa, waliotajwa majina yao, kwa kumushukuru Yawe kwa sababu wema wake unadumu milele.