1 Chronicles 17:10 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
tangu wakati nilipowateua waamuzi juu ya watu wangu Israeli; mimi nitawashinda maadui zako wote. Zaidi ya yote, mimi Mwenyezi-Mungu nakutangazia kuwa nitakujengea nyumba.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
na ambavyo wamefanya siku zote tangu nilipowachagua viongozi kwa ajili ya watu wangu Israeli. Pia nitawatiisha adui zenu wote. “ ‘Pamoja na hayo ninakuambia kwamba Mwenyezi Mungu atakujengea nyumba:
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na tangu siku ile nilipowaamuru waamuzi wawe juu ya watu wangu Israeli, nami nitawashinda adui zako wote. Pamoja na hayo nakuambia, ya kwamba Bwana atakujengea nyumba.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
tangu wakati nilipowateua waamuzi juu ya watu wangu Israeli; mimi nitawashinda maadui zako wote. Zaidi ya yote, mimi Mwenyezi-Mungu nakutangazia kuwa nitakujengea nyumba.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
na ambavyo wamefanya siku zote tangu nilipowachagua viongozi kwa ajili ya watu wangu Israeli. Pia nitawatiisha adui zenu wote. “ ‘Pamoja na hayo ninakuambia kwamba BWANA atakujengea nyumba:
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
na ambavyo wamefanya siku zote tangu nilipowachagua viongozi kwa ajili ya watu wangu Israeli. Pia nitawatiisha adui zenu wote. “ ‘Pamoja na hayo ninakuambia kwamba bwana atakujengea nyumba:
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na tangu siku ile nilipowaamuru waamuzi wawatawale watu wangu Israeli, nami nitawashinda adui zako wote. Pamoja na hayo nakuambia, ya kwamba BWANA atakujengea nyumba.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
tangu wakati nilipowateua waamuzi juu ya watu wangu Israeli; mimi nitawashinda maadui zako wote. Zaidi ya yote, mimi Mwenyezi-Mungu nakutangazia kuwa nitakujengea nyumba.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
tangu siku zile nilipowaagiza waamuzi, wawatawale walio ukoo wangu wa Waisiraeli; nitawanyenyekeza adui zako wote, tena ninakuambia sasa: Bwana atakujengea nyumba.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na tangu siku ile nilipowaamuru waamuzi wawe juu ya watu wangu Israeli, nami nitawashinda adui zako wote. Pamoja na hayo nakuambia, ya kwamba BWANA atakujengea nyumba.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
wakati nilipowachagua waamuzi juu ya watu wangu Waisraeli. Mimi nitawashinda waadui zako wote. Zaidi ya yote, mimi Yawe ninakutangazia kwamba nitakupa wazao.