1 Chronicles 17:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku zako zitakapotimia za kujiunga na babu zako, nitamfanya mmoja wa watoto wako, wewe mwenyewe awe mfalme; nami nitauimarisha ufalme wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Siku zako zikiisha, nawe ukaenda kulala na baba zako, nitamwinua mzao wako kuwa mfalme baada yako, mmoja wa wana wako mwenyewe, nami nitauimarisha ufalme wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata itakuwa, siku zako zitakapotimia, uende na babazo, nitainua mzao wako nyuma yako, atakayekuwa wa wana wako; nami nitaufanya imara ufalme wake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku zako zitakapotimia za kujiunga na babu zako, nitamfanya mmoja wa watoto wako, wewe mwenyewe awe mfalme; nami nitauimarisha ufalme wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati wako utakapokuwa umekwisha, nawe ukawa umekwenda kukaa na baba zako, nitamwinua mzao wako aingie mahali pako kuwa mfalme, mmoja wa wana wako mwenyewe, nami nitaufanya imara ufalme wake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati wako utakapokuwa umekwisha, nawe ukawa umekwenda kukaa na baba zako, nitamwinua mzao wako aingie mahali pako kuwa mfalme, mmoja wa wana wako mwenyewe, nami nitaufanya imara ufalme wake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata itakuwa, siku zako zitakapotimia, uende kulala pamoja na baba zako, nitainua mzawa wako nyuma yako, atakayekuwa wa wana wako; nami nitauimarisha ufalme wake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku zako zitakapotimia za kujiunga na babu zako, nitamfanya mmoja wa watoto wako, wewe mwenyewe awe mfalme; nami nitauimarisha ufalme wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Itakuwa hapo, siku zako zitakapotimia, uende kulala pamoja na baba zako; ndipo, nitakapoinua nyuma yako mzao wako atakayetoka kwa wanao, niusimike ufalme wake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata itakuwa, siku zako zitakapotimia, uende na babazo, nitainua mzao wako nyuma yako, atakayekuwa wa wana wako; nami nitaufanya imara ufalme wake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku zako zitakapotimia za kujiunga na babu zako, nitamufanya mumoja wa watoto wako wewe mwenyewe akuwe mufalme; nami nitaimarisha ufalme wake.