1 Chronicles 17:16 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha mfalme Daudi akaingia ndani ya hema na kuketi mbele ya Mwenyezi-Mungu, halafu akaomba, “Mimi ni nani, ee Mwenyezi-Mungu, na nyumba yangu ni nini hata unitukuze hivi?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Mfalme Daudi akaingia ndani, akaketi mbele za Mwenyezi Mungu, akasema: “Mimi ni nani, Ee Bwana Mwenyezi Mungu, na jamaa yangu ni nini, hata umenileta hadi hapa?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo akaingia Daudi mfalme, akaketi mbele za Bwana; akasema Mimi ni nani, Ee Bwana Mungu, na nyumba yangu ni nini, hata umenileta hata hapa?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha mfalme Daudi akaingia ndani ya hema na kuketi mbele ya Mwenyezi-Mungu, halafu akaomba, “Mimi ni nani, ee Mwenyezi-Mungu, na nyumba yangu ni nini hata unitukuze hivi?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Mfalme Daudi akaingia ndani akaketi mbele za BWANA akasema: “Mimi ni nani, Ee BWANA Mungu na jamaa yangu ni nini, hata unitendee haya yote?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Mfalme Daudi akaingia ndani, akaketi mbele za bwana, akasema: “Mimi ni nani, Ee bwana Mwenyezi Mungu, na jamaa yangu ni nini, hata umenileta mpaka hapa nilipo?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo akaingia Daudi mfalme, akaketi mbele za BWANA; akasema Mimi ni nani, Ee BWANA Mungu, na nyumba yangu ni nini, hata umenileta hadi hapa?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha mfalme Daudi akaingia ndani ya hema na kuketi mbele ya Mwenyezi-Mungu, halafu akaomba, “Mimi ni nani, ee Mwenyezi-Mungu, na nyumba yangu ni nini hata unitukuze hivi?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha mfalme Dawidi akaingia pake Bwana, akakaa hapo akisema: Bwana Mungu, mimi ni nani? Nao mlango wangu ni nini ukinileta, nifike hapa?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo akaingia Daudi mfalme, akaketi mbele za BWANA; akasema Mimi ni nani, Ee BWANA Mungu, na nyumba yangu ni nini, hata umenileta hata hapa?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha mufalme Daudi akaingia ndani ya hema na kuikaa mbele ya Yawe, halafu akaomba: “Mimi ni nani, ee Yawe Mungu, na nyumba yangu ni nini hata unitukuze hivi?