1 Chronicles 17:21 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tena ni watu gani duniani ambao wanaweza kulinganishwa na watu wako wa Israeli ambao peke yao Mungu wao alikwenda kuwakomboa ili wawe watu wake? Wewe ulijifanyia jina kwa kutenda mambo makubwa na ya ajabu hapo ulipoyafukuza mataifa mbele ya watu wako ambao uliwakomboa kutoka Misri.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Naye ni nani aliye kama watu wako Israeli: taifa pekee duniani ambalo Mungu wake alitoka kwenda kulikomboa kwa ajili yake mwenyewe, na kujifanyia jina kwa ajili yake mwenyewe, na kufanya maajabu makubwa na ya kutisha, kwa kuwafukuza mataifa mbele ya watu wako, ambao uliwakomboa kutoka Misri?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena ni taifa lipi duniani lililo kama watu wako Israeli, ambalo Mungu alikwenda kuwakomboa kwa ajili yake mwenyewe, ili wawe watu wake, na kujifanyia jina kwa njia ya mambo makuu, yenye kuogofya, kwa kufukuza mataifa mbele ya watu wako, uliowakomboa kutoka Misri?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tena ni watu gani duniani ambao wanaweza kulinganishwa na watu wako wa Israeli ambao peke yao Mungu wao alikwenda kuwakomboa ili wawe watu wake? Wewe ulijifanyia jina kwa kutenda mambo makubwa na ya ajabu hapo ulipoyafukuza mataifa mbele ya watu wako ambao uliwakomboa kutoka Misri.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Naye ni nani aliye kama watu wako Israeli, taifa moja duniani ambalo Mungu wake alitoka kwenda kulikomboa kwa ajili yake mwenyewe na kujifanyia jina kwa ajili yake mwenyewe, wa kufanya maajabu makubwa ya kutisha kwa kuwafukuza mataifa mbele ya watu wako, uliowakomboa kutoka Misri?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Naye ni nani aliye kama watu wako Israeli: taifa pekee duniani ambalo Mungu wake alitoka kwenda kulikomboa kwa ajili yake mwenyewe na kujifanyia jina kwa ajili yake mwenyewe, kwa kufanya maajabu makubwa na ya kutisha kwa kuwafukuza mataifa mbele ya watu wako, ambao uliwakomboa kutoka Misri?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena ni taifa lipi duniani lililo kama watu wako Israeli, ambalo Mungu alikwenda kuwakomboa kwa ajili yake mwenyewe, ili wawe watu wake, na kujifanyia jina kwa njia ya mambo makuu, yenye kuogofya, kwa kufukuza mataifa mbele ya watu wako, uliowakomboa kutoka Misri?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tena ni watu gani duniani ambao wanaweza kulinganishwa na watu wako wa Israeli ambao peke yao Mungu wao alikwenda kuwakomboa ili wawe watu wake? Wewe ulijifanyia jina kwa kutenda mambo makubwa na ya ajabu hapo ulipoyafukuza mataifa mbele ya watu wako ambao uliwakomboa kutoka Misri.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena liko taifa moja tu huku nchini linalofanana na ukoo wako wa Waisiraeli? Hao ndio, Mungu aliokwenda kuwakomboa, wawe ukoo wake. Hapo ulijipatia Jina kwa matendo makubwa yaliyoogopesha, ulipowafukuza wamizimu mbele yao walio ukoo wako, uliowakomboa na kuwatoa Misri.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena ni taifa lipi duniani lililo kama watu wako Israeli, ambalo Mungu alikwenda kuwakomboa kwa ajili yake mwenyewe, ili wawe watu wake, na kujifanyia jina kwa njia ya mambo makuu, yenye kuogofya, kwa kufukuza mataifa mbele ya watu wako, uliowakomboa kutoka Misri?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tena ni watu gani katika dunia ambao wanaweza kulinganishwa na watu wako Waisraeli? Hao ndio watu peke yao Mungu wao alikwenda kuwakomboa kusudi wakuwe watu wake. Ukajipatia sifa kwa kutenda mambo makubwa na ya ajabu pale ulipofukuza mataifa mbele ya watu wako ambao uliwakomboa kutoka Misri.