1 Chronicles 17:25 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana ee Mungu wangu nimepata ujasiri kukuomba kwa sababu wewe, umenifunulia ukisema ya kwamba utanijengea nyumba.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Wewe, Mungu wangu, umemfunulia mtumishi wako Daudi kwamba utamjengea nyumba. Hivyo mtumishi wako amekuwa na ujasiri wa kukuomba maombi haya.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa kuwa wewe, Ee Mungu wangu, umenifunulia mimi mtumwa wako ya kuwa utanijengea nyumba; kwa hiyo mimi mtumwa wako nimeona vema moyoni mwangu kuomba mbele yako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana ee Mungu wangu nimepata ujasiri kukuomba kwa sababu wewe, umenifunulia ukisema ya kwamba utanijengea nyumba.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Wewe, Mungu wangu, umemfunulia mtumishi wako Daudi kwamba utamjengea yeye nyumba. Hivyo mtumishi wako amekuwa na ujasiri wa kukuomba maombi haya.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Wewe, Mungu wangu, umemfunulia mtumishi wako Daudi kwamba utamjengea yeye nyumba. Hivyo mtumishi wako amekuwa na ujasiri wa kukuomba maombi haya.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa kuwa wewe, Ee Mungu wangu, umenifunulia mimi mtumishi wako ya kuwa utanijengea nyumba; kwa hiyo mimi mtumishi wako nimeona vema moyoni mwangu kuomba mbele yako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana ee Mungu wangu nimepata ujasiri kukuomba kwa sababu wewe, umenifunulia ukisema ya kwamba utanijengea nyumba.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani wewe, Mungu wangu, umelifunua sikio la mtumishi wako, asikie, ya kuwa utamjengea nyumba, kwa hiyo mtumishi wako ameiona njia hii ya kukutolea maombo haya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa kuwa wewe, Ee Mungu wangu, umenifunulia mimi mtumwa wako ya kuwa utanijengea nyumba; kwa hiyo mimi mtumwa wako nimeona vema moyoni mwangu kuomba mbele yako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Maana, ee Mungu wangu, nimepata bidii ya kukuomba kwa sababu umenifunulia ukisema kwamba utanipa wazao.