1 Chronicles 17:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tangu wakati ule nilipowaongoza watu wa Israeli kutoka Misri mpaka hivi leo, sijaishi kwenye nyumba. Nimekuwa nikihama toka hema hadi hema, na toka makao hadi makao mengine.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mimi sijakaa ndani ya nyumba tangu siku niliyowatoa Israeli kutoka Misri hadi leo. Nimehama kutoka hema moja hadi jingine, na kutoka mahali pamoja hadi pengine.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kwa maana sikukaa ndani ya nyumba tangu siku ile nilipowaleta Israeli huku hata leo; lakini hema kwa hema nimehamia, na maskani kwa maskani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tangu wakati ule nilipowaongoza watu wa Israeli kutoka Misri mpaka hivi leo, sijaishi kwenye nyumba. Nimekuwa nikihama toka hema hadi hema, na toka makao hadi makao mengine.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mimi sijakaa ndani ya nyumba tangu siku ile niliyowatoa Israeli kutoka Misri mpaka leo. Nimehama kutoka hema moja hadi jingine na kutoka mahali pamoja hadi pengine.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mimi sijakaa ndani ya nyumba tangu siku ile niliyowatoa Israeli kutoka Misri mpaka leo. Nimehama kutoka hema moja hadi jingine na kutoka mahali pamoja hadi pengine.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kwa maana sikukaa ndani ya nyumba tangu siku ile nilipowaleta Israeli huku hata leo; lakini hema kwa hema nimehamia, na maskani kwa maskani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tangu wakati ule nilipowaongoza watu wa Israeli kutoka Misri mpaka hivi leo, sijaishi kwenye nyumba. Nimekuwa nikihama toka hema hadi hema, na toka makao hadi makao mengine.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani sikukaa nyumbani tangu siku ile, nilipowaleta Waisiraeli huku milimani, mpaka siku hii ya leo, ila nilikuwa hemani huku, tena hamani huko, Kao langu likawa huku na huko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kwa maana sikukaa ndani ya nyumba tangu siku ile nilipowaleta Israeli huku hata leo; lakini hema kwa hema nimehamia, na maskani kwa maskani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tangu wakati ule nilipowaongoza watu wa Israeli kutoka Misri mpaka hivi leo, sijaishi katika nyumba. Nimekuwa nikihama toka hema hata hema, na toka makao hata makao mengine.