1 Chronicles 17:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Je, kila mahali ambako nimekwenda na Waisraeli, nimepata kumwuliza mwamuzi wao yeyote niliyemwamuru awachunge watu wangu, “Kwa nini hukunijengea nyumba ya mierezi?” ’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Popote nilipoenda pamoja na Waisraeli wote, je, kuna wakati nilimuuliza kiongozi yeyote niliyemwagiza kuwachunga watu wangu, “Kwa nini hujanijengea nyumba ya mwerezi?” ’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Katika mahali mwote nilimokwenda na Israeli wote, je! Nimesema neno lo lote na mtu ye yote wa waamuzi wa Israeli, niliowaagiza kuwalisha watu wangu, nikisema, Mbona hamkunijengea nyumba ya mwerezi?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Je, kila mahali ambako nimekwenda na Waisraeli, nimepata kumwuliza mwamuzi wao yeyote niliyemwamuru awachunge watu wangu, “Kwa nini hukunijengea nyumba ya mierezi?”’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Je, po pote nilipokwenda pamoja na Waisraeli wote, wakati wo wote nilimwambia kiongozi ye yote niliyemwagiza kuwachunga watu wangu, kwa nini hujanijengea nyumba ya mierezi?’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Je, popote nilipokwenda pamoja na Waisraeli wote, wakati wowote nilimwambia kiongozi yeyote niliyemwagiza kuwachunga watu wangu, kwa nini hujanijengea nyumba ya mierezi?’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kila mahali nilikokwenda na Israeli wote, je! Nimesema neno lolote na mtu yeyote wa waamuzi wa Israeli, niliowaagiza kuwalisha watu wangu, nikisema, Mbona hamkunijengea nyumba ya mwerezi?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Je, kila mahali ambako nimekwenda na Waisraeli, nimepata kumwuliza mwamuzi wao yeyote niliyemwamuru awachunge watu wangu, “Kwa nini hukunijengea nyumba ya mierezi?” ’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Je? Hapo pote, nilipokwenda pamoja na Waisiraeli wote, nilimwambia hata mmoja wao waamuzi wa Waisiraeli, niliowaagiza kuwachunga walio ukoo wangu, na kumwuliza neno la kwamba: Mbona hamnijengei nyumba ya miangati?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Katika mahali mwote nilimokwenda na Israeli wote, je! Nimesema neno lo lote na mtu ye yote wa waamuzi wa Israeli, niliowaagiza kuwalisha watu wangu, nikisema, Mbona hamkunijengea nyumba ya mwerezi?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kila pahali nilipokwenda na Waisraeli, sikupata hata mara moja kuwauliza waamuzi wao niliowaamuru wachunge watu wangu, ‘Kwa nini haukunijengea nyumba ya mierezi?’