1 Chronicles 17:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa hiyo basi, mwambie mtumishi wangu Daudi: ‘Mwenyezi-Mungu wa majeshi anasema hivi: Nilikutoa malishoni ulipokuwa unawachunga kondoo, ili uwe mkuu wa watu wangu Israeli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Sasa basi, mwambie mtumishi wangu Daudi, ‘Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: Nilikutoa malishoni na kutoka kulisha mifugo, ili uwaongoze watu wangu Israeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi sasa ndivyo utakavyomwambia mtumishi wangu Daudi, Bwana wa majeshi asema hivi, Nalikutwaa katika zizi la kondoo, katika kuwaandama kondoo ili uwe mkuu juu ya watu wangu Israeli;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa hiyo basi, mwambie mtumishi wangu Daudi: ‘Mwenyezi-Mungu wa majeshi anasema hivi: Nilikutoa malishoni ulipokuwa unawachunga kondoo, ili uwe mkuu wa watu wangu Israeli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Sasa basi, mwambie mtumishi wangu Daudi, ‘Hili ndilo asemalo BWANA Mwenye Nguvu Zote: Nilikuchukua machungani na kutoka kuandama kondoo ili uwatawale watu wangu Israeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Sasa basi, mwambie mtumishi wangu Daudi, ‘Hili ndilo asemalo bwana Mwenye Nguvu Zote: Nilikuchukua machungani na kutoka kuandama kondoo ili uwatawale watu wangu Israeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi sasa ndivyo utakavyomwambia mtumishi wangu Daudi, BWANA wa majeshi asema hivi, Nilikutwaa kutoka machungani, hata katika kuwafuata kondoo ili uwe mkuu juu ya watu wangu Israeli;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa hiyo basi, mwambie mtumishi wangu Daudi: ‘Mwenyezi-Mungu wa majeshi anasema hivi: Nilikutoa malishoni ulipokuwa unawachunga kondoo, ili uwe mkuu wa watu wangu Israeli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
kwa hiyo umwambie sasa mtumishi wangu Dawidi: Hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi anavyosema: Mimi nilikuchukua malishoni, ulipowafuata kondoo, uwe nwenye kuwatawala walio ukoo wangu wa Waisiraeli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi sasa ndivyo utakavyomwambia mtumishi wangu Daudi, BWANA wa majeshi asema hivi, Nalikutwaa katika zizi la kondoo, katika kuwaandama kondoo ili uwe mkuu juu ya watu wangu Israeli;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Kwa hiyo basi, umwambie mutumishi wangu Daudi: Yawe wa majeshi anasema hivi: Nilikutoa katika shamba la malisho ulipokuwa unachunga kondoo, kusudi ukuwe mukubwa wa watu wangu Waisraeli.