1 Chronicles 17:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tangu wakati huo nimekuwa pamoja nawe kokote ulikokwenda na nimewaangamiza maadui zako wote mbele yako. Nitakufanya kuwa maarufu kama wakuu wengine wa dunia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nimekuwa pamoja nawe popote ulipoenda, nami nimekuondolea mbali adui zako wote mbele yako. Basi nitalifanya jina lako kuwa kuu kama majina ya watu walio wakuu sana duniani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
nami nimekuwa pamoja nawe kila ulikokwenda, na kuwakatilia mbali adui zako wote mbele yako; nami nitakufanyia jina, kama jina la hao wakuu walioko duniani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tangu wakati huo nimekuwa pamoja nawe kokote ulikokwenda na nimewaangamiza maadui zako wote mbele yako. Nitakufanya kuwa maarufu kama wakuu wengine wa dunia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nimekuwa pamoja nawe po pote ulipokwenda, nami nimewakatilia mbali adui zako wote mbele yako. Basi nitalifanya jina lako kuwa kama majina ya watu wengine wakuu sana wa dunia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nimekuwa pamoja nawe popote ulipokwenda, nami nimekuondolea mbali adui zako wote mbele yako. Basi nitalifanya jina lako kuwa kuu kama majina ya watu walio wakuu sana duniani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
nami nimekuwa pamoja nawe kila ulikokwenda, na kuwakatilia mbali adui zako wote mbele yako; nami nitakufanyia jina, kama jina la hao wakuu walioko duniani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tangu wakati huo nimekuwa pamoja nawe kokote ulikokwenda na nimewaangamiza maadui zako wote mbele yako. Nitakufanya kuwa maarufu kama wakuu wengine wa dunia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nikawa pamoja na wewe po pote, ulipokwenda, nikawaangamiza adui zako wote mbele yako; nitakupatia jina lililo sawa na majina ya wakubwa walioko huku nchini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
nami nimekuwa pamoja nawe kila ulikokwenda, na kuwakatilia mbali adui zako wote mbele yako; nami nitakufanyia jina, kama jina la hao wakuu walioko duniani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tangu wakati ule nimekuwa pamoja nawe kokote ulikokwenda na nimewaangamiza waadui zako wote mbele yako. Nitakufanya kuwa mwenye heshima kama vile wakubwa wengine wa dunia.