1 Chronicles 18:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Daudi pia alimshinda Hadadezeri mfalme wa Soba, nchi iliyokuwa karibu na Hamathi, alifanya hivyo wakati alipokuwa akienda kujisimamishia nguzo ya kumbukumbu kwenye sehemu za mto Eufrate.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Zaidi ya hayo, Daudi akapigana na Hadadezeri mfalme wa Soba, hadi Hamathi, wakati alienda kuimarisha utawala wake katika Mto Frati.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena Daudi akampiga Hadadezeri, mfalme wa Soba, mpaka Hamathi, alipokwenda kujisimamishia mamlaka yake kwenye mto wa Frati.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Daudi pia alimshinda Hadadezeri mfalme wa Soba, nchi iliyokuwa karibu na Hamathi, alifanya hivyo wakati alipokuwa akienda kujisimamishia nguzo ya kumbukumbu kwenye sehemu za mto Eufrate.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Zaidi ya hayo, Daudi akapigana na Hadadezeri mfalme wa Soba, hadi Hamathi, wakati alipokwenda kuimarisha utawala wake katika Mto Eufrati.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Zaidi ya hayo, Daudi akapigana na Hadadezeri mfalme wa Soba, hadi Hamathi, wakati alikwenda kuimarisha utawala wake katika Mto Frati.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena Daudi akampiga Hadadezeri, mfalme wa Soba, mpaka Hamathi, alipokwenda kujisimamishia mnara wa ukumbusho kwenye mto wa Frati.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Daudi pia alimshinda Hadadezeri mfalme wa Soba, nchi iliyokuwa karibu na Hamathi, alifanya hivyo wakati alipokuwa akienda kujisimamishia nguzo ya kumbukumbu kwenye sehemu za mto Eufrate.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Dawidi akampiga Hadarezeri, mfalme wa Soba ulioko upande wa Hamati, alipokwenda kuusimika tena ufalme wake huko kwenye jito la Furati.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena Daudi akampiga Hadadezeri, mfalme wa Soba, mpaka Hamathi, alipokwenda kujisimamishia mamlaka yake kwenye mto wa Frati.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Daudi akamushinda vilevile Hadadezeri mufalme wa Zoba, inchi iliyokuwa karibu na Hamati, alifanya hivyo wakati alipokuwa akienda kujisimamishia nguzo ya ukumbusho kwenye sehemu za muto Furati.