1 Chronicles 18:4 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Daudi akateka magari ya farasi 1,000, askari wapandafarasi 7,000 na wa miguu 20,000. Kisha Daudi alikata mishipa ya miguu ya nyuma ya farasi wote wa magari, ila aliwabakiza 100.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Daudi akateka magari ya vita elfu moja miongoni mwa magari yake, waendesha hayo magari ya vita elfu saba, na askari wa miguu elfu ishirini. Daudi akakata mishipa ya miguu ya farasi wa magari ya vita, akabakiza farasi mia moja.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Daudi akampokonya magari elfu, na wapanda farasi saba elfu, na askari waendao kwa miguu ishirini elfu; Daudi akawakata mshipa farasi wote wa magari, ila wa magari mia akawaweka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Daudi akateka magari ya farasi 1,000, askari wapandafarasi 7,000 na wa miguu 20,000. Kisha Daudi alikata mishipa ya miguu ya nyuma ya farasi wote wa magari, ila aliwabakiza 100.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Daudi akateka magari ya vita 1,000 miongoni mwa magari yake, waendesha hayo magari ya kukokotwa na farasi 7,000 na askari wa miguu 20,000. Daudi akakata mishipa ya miguu ya nyuma ya farasi wote wakokotao magari, ila akabakiza 100.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Daudi akateka magari ya vita 1,000 miongoni mwa magari yake, waendesha hayo magari ya kukokotwa na farasi 7,000 na askari wa miguu 20,000. Daudi akakata mishipa ya miguu ya nyuma ya farasi wote wakokotao magari, ila akabakiza 100.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Daudi akampokonya magari elfu moja, na wapanda farasi elfu saba, na askari waendao kwa miguu elfu ishirini; Daudi akawakata mshipa farasi wote wa magari, ila wa magari mia moja akawaweka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Daudi akateka magari ya farasi 1,000, askari wapandafarasi 7,000 na wa miguu 20,000. Kisha Daudi alikata mishipa ya miguu ya nyuma ya farasi wote wa magari, ila aliwabakiza 100.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Dawidi akateka kwake magari 1000, na wapanda farasi 7000 na askari waliokwenda kwa miguu 20000, nao farasi wote wa kuvuta magari Dawidi akawakata mishipa ya miguu, akajisazia farasi wa magari mia tu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Daudi akampokonya magari elfu, na wapanda farasi saba elfu, na askari waendao kwa miguu ishirini elfu; Daudi akawakata mshipa farasi wote wa magari, ila wa magari mia akawaweka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Daudi akanyanganya magari ya vita elfu moja, waaskari wapanda-farasi elfu saba na wa miguu elfu makumi mbili. Kisha Daudi akakata mishipa ya miguu ya nyuma ya farasi wote wa magari, lakini akaacha mia moja.