1 Chronicles 18:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Halafu Daudi aliweka kambi za kijeshi katika mji wa Shamu ya Damasko. Basi Waaramu wakawa watumishi wake, na wakawa wanalipa kodi. Mwenyezi-Mungu alimpa Daudi ushindi kokote alikokwenda.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Daudi akaweka askari walinzi katika ufalme wa Waaramu huko Dameski. Basi Waaramu wakawa watumwa wa Daudi, na kumlipa ushuru. Mwenyezi Mungu akampa Daudi ushindi kote alipoenda.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo Daudi akaweka ngome katika Shamu ya Dameski; nao Washami wakawa watumwa wa Daudi, wakaleta zawadi. Naye Bwana akampa Daudi kushinda kila alikokwenda.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Halafu Daudi aliweka kambi za kijeshi katika mji wa Shamu ya Damasko. Basi Waaramu wakawa watumishi wake, na wakawa wanalipa kodi. Mwenyezi-Mungu alimpa Daudi ushindi kokote alikokwenda.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Daudi akaweka askari walinzi katika ufalme wa Waaramu huko Dameski. Basi Waaramu wakawa watumishi wa Daudi, wakawa wanamletea ushuru. BWANA akampa Daudi ushindi kila mahali alipokwenda.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Daudi akaweka askari walinzi katika ufalme wa Waaramu huko Dameski. Basi Waaramu wakawa watumwa wa Daudi, na kumlipa ushuru. bwana akampa Daudi ushindi kote alipokwenda.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo Daudi akaweka ngome katika Shamu ya Dameski; nao Washami wakawa watumwa wa Daudi, wakaleta zawadi. Naye BWANA akampa Daudi kushinda kila alikokwenda.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Halafu Daudi aliweka kambi za kijeshi katika mji wa Shamu ya Damasko. Basi Waaramu wakawa watumishi wake, na wakawa wanalipa kodi. Mwenyezi-Mungu alimpa Daudi ushindi kokote alikokwenda.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Dawidi akaweka askari kwao Washami wa Damasko, hao Washami wakawa watumishi wa Dawidi, wakamletea mahongo. Ndivyo, Bwana alivyompa Dawidi kushinda pote, alipokwenda.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo Daudi akaweka ngome katika Shamu ya Dameski; nao Washami wakawa watumwa wa Daudi, wakaleta zawadi. Naye BWANA akampa Daudi kushinda kila alikokwenda.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu Daudi akaweka kambi za waaskari katika muji wa Damasiki wa Aramu. Basi Waaramu wakakuwa watumishi wake, na wakakuwa wanalipa kodi. Yawe akamupa Daudi ushindi kokote alikokwenda.