1 Chronicles 18:8 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Daudi alichukua pia shaba nyingi sana kutoka mji wa Tibhathi na mji wa Kuni; iliyokuwa miji ya Hadadezeri. Solomoni aliitumia shaba hiyo kutengenezea nguzo na vyombo vya shaba.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kutoka miji ya Tibathi na Kuni, iliyokuwa miji ya Hadadezeri, Daudi akatwaa shaba nyingi sana, ambayo Sulemani aliitumia kutengenezea ile Bahari ya shaba, zile nguzo na vifaa mbalimbali vya shaba.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena toka Tibhathi, na toka Berothai, miji ya Hadadezeri, Daudi akatwaa shaba nyingi mno, aliyofanyizia Sulemani ile bahari ya shaba, na zile nguzo, na vile vyombo vya shaba.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Daudi alichukua pia shaba nyingi sana kutoka mji wa Tibhathi na mji wa Kuni; iliyokuwa miji ya Hadadezeri. Solomoni aliitumia shaba hiyo kutengenezea nguzo na vyombo vya shaba.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kutoka mji wa Tibhathi na mji wa Kuni, iliyokuwa miji ya Hadadezeri, Daudi akachukua pia shaba nyingi sana, ambayo Solomoni aliitumia kutengenezea ile Bahari ya shaba, zile nguzo na vifaa mbalimbali vya shaba.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kutoka miji ya Tibhathi na Kuni, iliyokuwa miji ya Hadadezeri, Daudi akatwaa shaba nyingi sana, ambayo Sulemani aliitumia kutengenezea ile Bahari ya shaba, zile nguzo na vifaa mbalimbali vya shaba.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena toka Tibhathi, na toka Berothai, miji ya Hadadezeri, Daudi akatwaa shaba nyingi mno, aliyoitumia Sulemani katika kutengeneza lile birika la shaba, na zile nguzo, na vile vyombo vya shaba.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Daudi alichukua pia shaba nyingi sana kutoka mji wa Tibhathi na mji wa Kuni; iliyokuwa miji ya Hadadezeri. Solomoni aliitumia shaba hiyo kutengenezea nguzo na vyombo vya shaba.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Namo mle Tibehati na Kuni iliyokuwa miji ya Hadarezeri Dawidi akachukua shaba nyekundu nyingi mno; ndizo, Salomo alizozitumia za kutengeneza ile bahari ya shaba nazo zile nguzo navyo vyombo vya shaba.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena toka Tibhathi, na toka Berothai, miji ya Hadadezeri, Daudi akatwaa shaba nyingi mno, aliyofanyizia Sulemani ile bahari ya shaba, na zile nguzo, na vile vyombo vya shaba.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Daudi alichukua vilevile shaba nyingi sana kutoka muji wa Tibuhati na muji wa Kuni iliyokuwa miji ya Hadadezeri. Solomono alitumia shaba hiyo kwa kutengeneza nguzo na vyombo vya shaba.