1 Chronicles 19:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yoabu alipoona kuwa vita ni vikali dhidi yake, mbele na nyuma, aliwateua baadhi ya wanajeshi hodari zaidi wa Waisraeli, akawapanga kukabiliana na Waaramu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yoabu akaona kuwa mbele yake na nyuma yake kumepangwa vita; kwa hiyo akachagua baadhi ya vikosi vilivyo bora sana katika Israeli, akavipanga dhidi ya Waaramu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Yoabu alipoona ya kwamba uso wa vita umekuwa juu yake mbele na nyuma, akachagua baadhi ya wateule wote wa Israeli, akawapanga juu ya Washami.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yoabu alipoona kuwa vita ni vikali dhidi yake, mbele na nyuma, aliwateua baadhi ya wanajeshi hodari zaidi wa Waisraeli, akawapanga kukabiliana na Waaramu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yoabu akaona kwamba jeshi limejipanga mbele yake na nyuma yake, kwa hiyo akachagua baadhi ya vikosi bora katika Israeli na kuvipanga dhidi ya Waaramu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yoabu akaona kuwa mbele yake na nyuma yake kumepangwa vita; kwa hiyo akachagua baadhi ya vikosi vilivyo bora sana katika Israeli akavipanga dhidi ya Waaramu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Yoabu alipoona ya kwamba wamejipanga kwa vita juu yake mbele na nyuma, akachagua baadhi ya wateule wote wa Israeli, akawapanga juu ya Washami.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yoabu alipoona kuwa vita ni vikali dhidi yake, mbele na nyuma, aliwateua baadhi ya wanajeshi hodari zaidi wa Waisraeli, akawapanga kukabiliana na Waaramu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yoabu alipoona, ya kuwa wamejipanga kupiga vita usoni na mgongoni kwake, akachagua wengine katika wateule wote wa Waisiraeli, akawapanga, wapigane na Washami.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Yoabu alipoona ya kwamba uso wa vita umekuwa juu yake mbele na nyuma, akachagua baadhi ya wateule wote wa Israeli, akawapanga juu ya Washami.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yoabu alipoona kwamba vita ni kali juu yake, mbele na nyuma, akachagua waaskari hodari zaidi kati ya Waisraeli, akawapanga mbele ya Waaramu.