1 Chronicles 19:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yoabu akamwambia Abishai, “Ikiwa Waaramu wananizidi nguvu, utanisaidia; lakini kama Waamoni wanakuzidi nguvu, nitakuja kukusaidia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yoabu akasema, “Kama Waaramu watanizidi nguvu, basi itakupasa wewe uniokoe; lakini kama Waamoni watakuzidi nguvu, basi mimi nitakuokoa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akasema, Wakiwa Washami ni hodari mno kwangu, ndipo wewe utanisaidia; lakini wana wa Amoni wakiwa ni hodari mno kwako, ndipo mimi nitakusaidia wewe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yoabu akamwambia Abishai, “Ikiwa Waaramu wananizidi nguvu, utanisaidia; lakini kama Waamoni wanakuzidi nguvu, nitakuja kukusaidia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yoabu akasema, “Kama Waamoni watanizidi nguvu, basi itakupasa wewe unisaidie, lakini kama Waamoni watakuzidi nguvu, basi mimi nitakusaidia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yoabu akasema, “Kama Waaramu watanizidi nguvu, basi itakupasa wewe unisaidie; lakini kama Waamoni watakuzidi nguvu, basi mimi nitakusaidia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akasema, Washami wakiwa ni hodari mno kwangu, ndipo wewe utanisaidia; lakini wana wa Amoni wakiwa ni hodari mno kwako, ndipo mimi nitakusaidia wewe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yoabu akamwambia Abishai, “Ikiwa Waaramu wananizidi nguvu, utanisaidia; lakini kama Waamoni wanakuzidi nguvu, nitakuja kukusaidia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
akasema: Kama Washami wanapata nguvu za kunishinda, sharti uje kunisaidia. Tena kama wana wa Amoni wanapata nguvu za kukushinda, sharti nije, nikusaidie.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akasema, Wakiwa Washami ni hodari mno kwangu, ndipo wewe utanisaidia; lakini wana wa Amoni wakiwa ni hodari mno kwako, ndipo mimi nitakusaidia wewe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yoabu akamwambia Abisai: “Ikiwa Waaramu wananizidi nguvu, utanisaidia; lakini kama Waamoni wanakuzidi nguvu, nitakuja kukusaidia.