1 Chronicles 19:17 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Daudi alipopata habari, aliwakusanya pamoja Waisraeli wote, akavuka mto Yordani, akawaendea, akapanga vikosi vyake dhidi yao. Daudi alipopanga vita dhidi ya Wasiria, basi nao walipigana naye.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Daudi alipoambiwa haya, akawakusanya Israeli wote na kuvuka Yordani. Akasonga mbele dhidi yao na akajipanga kuwakabili. Daudi akapanga vita ili kupigana na Waaramu, nao wakapigana dhidi yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Alipoambiwa Daudi; akakusanya Israeli wote, akavuka Yordani, akawajia, akapanga vita juu yao. Basi Daudi alipopanga vita juu ya Washami, wakapigana naye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Daudi alipopata habari, aliwakusanya pamoja Waisraeli wote, akavuka mto Yordani, akawaendea, akapanga vikosi vyake dhidi yao. Daudi alipopanga vita dhidi ya Wasiria, basi nao walipigana naye.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Daudi alipoelezwa haya, akawakusanya Israeli wote na kuvuka Yordani. Akasonga mbele dhidi yao na akajipanga kuwakabili. Daudi akapanga vita ili kupigana na Waaramu, nao wakapigana dhidi yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Daudi alipoambiwa haya, akawakusanya Israeli wote na kuvuka Yordani. Akasonga mbele dhidi yao na akajipanga kuwakabili. Daudi akapanga vita ili kupigana na Waaramu, nao wakapigana dhidi yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Alipoambiwa Daudi; akawakusanya Israeli wote, akavuka Yordani, akawajia, akapanga vita juu yao. Basi Daudi alipopanga vita juu ya Washami, wakapigana naye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Daudi alipopata habari, aliwakusanya pamoja Waisraeli wote, akavuka mto Yordani, akawaendea, akapanga vikosi vyake dhidi yao. Daudi alipopanga vita dhidi ya Wasiria, basi nao walipigana naye.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Dawidi alipopashwa habari hizo, akawakusanya Waisiraeli wote, akauvuka Yordani, akawajia, akajipanga mbele yao. Dawidi alipokwisha kujipanga kupiga vita na Washami, wakapigana naye.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Alipoambiwa Daudi; akakusanya Israeli wote, akavuka Yordani, akawajia, akapanga vita juu yao. Basi Daudi alipopanga vita juu ya Washami, wakapigana naye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Daudi alipopata habari, akakusanya pamoja Waisraeli wote, akavuka muto Yordani, akawaendea, akapanga vikundi vyake mbele yao. Daudi alipopanga vita juu ya Wasuria, basi nao wakapigana naye.