1 Chronicles 19:18 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Waaramu walikimbia mbele ya Waisraeli. Daudi aliwaua Waaramu waendeshao magari 7,000 na askari wa miguu 40,000. Pia alimuua Shofaki, kamanda wa jeshi lao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Waaramu wakakimbia mbele ya Israeli, naye Daudi akawaua waendesha magari ya vita elfu saba, na askari wa miguu elfu arobaini. Pia akamuua Shofaki, jemadari wa jeshi lao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Washami wakakimbia mbele ya Israeli; naye Daudi akawaua katika Washami watu wa magari saba elfu, na askari waendao kwa miguu arobaini elfu, akamwua na Shobaki, jemadari wa jeshi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Waaramu walikimbia mbele ya Waisraeli. Daudi aliwaua Waaramu waendeshao magari 7,000 na askari wa miguu 40,000. Pia alimuua Shofaki, kamanda wa jeshi lao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini walikimbia mbele ya Israeli, Daudi akawaua waendesha magari 7,000 na askari wao wa miguu 40,000. Pia akamwua Shofaki, jemadari wa jeshi lao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Waaramu wakakimbia mbele ya Israeli, naye Daudi akawaua waendesha magari 7,000 na askari wao wa miguu 40,000. Pia akamuua Shofaki, jemadari wa jeshi lao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Washami wakakimbia mbele ya Israeli; naye Daudi akawaua katika Washami watu wa magari elfu saba, na askari waendao kwa miguu elfu arobaini, akamwua na Shobaki, jemadari wa jeshi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Waaramu walikimbia mbele ya Waisraeli. Daudi aliwaua Waaramu waendeshao magari 7,000 na askari wa miguu 40,000. Pia alimuua Shofaki, kamanda wa jeshi lao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Washami wakawakimbia Waisiraeli, Dawidi akaua kwao Washamu watu 7000 waliopanda magari na watu 40000 waliokwenda kwa miguu, hata Sofaki, mkuu wa vikosi, akamwua.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Washami wakakimbia mbele ya Israeli; naye Daudi akawaua katika Washami watu wa magari saba elfu, na askari waendao kwa miguu arobaini elfu, akamwua na Shobaki, jemadari wa jeshi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Waaramu wakakimbia mbele ya Waisraeli. Daudi akawaua Waaramu wanaoendesha magari elfu saba na waaskari wa miguu elfu makumi ine. Vilevile akamwua Sofaki, jemadari wa jeshi lao.