1 Chronicles 19:2 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Daudi akasema, “Nitamtendea mema Hanuni mwana wa Nahashi, kwani baba yake alinitendea mema pia.” Hivyo Daudi alituma wajumbe na kumpelekea salamu za rambirambi kwa ajili ya kifo cha baba yake. Nao wakaenda kwa Hanuni ili kumfariji, huko katika nchi ya Waamoni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Daudi akawaza, “Nitamtendea wema Hanuni mwana wa Nahashi, kwa sababu baba yake alinitendea wema.” Hivyo Daudi akatuma wajumbe ili kumfariji Hanuni kwa ajili ya kifo cha baba yake. Watu wa Daudi walipofika kwa Hanuni katika nchi ya Waamoni ili kumfariji,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Daudi akasema, Nitamtendea wema Hanuni, mwana wa Nahashi, kwa kuwa babaye alinitendea mimi wema. Basi Daudi akapeleka wajumbe ili kumtuliza kwa habari za babaye. Wakaja watumishi wa Daudi katika nchi ya wana wa Amoni kwa Hanuni, ili wamtulize.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Daudi akasema, “Nitamtendea mema Hanuni mwana wa Nahashi, kwani baba yake alinitendea mema pia.” Hivyo Daudi alituma wajumbe na kumpelekea salamu za rambirambi kwa ajili ya kifo cha baba yake. Nao wakaenda kwa Hanuni ili kumfariji, huko katika nchi ya Waamoni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Daudi akawaza, “Nitamtendea mema Hanuni mwana wa Nahashi, kwa sababu baba yake alinitendea mema.” Hivyo Daudi akatuma wajumbe ili kumfariji Hanuni kwa ajili ya kifo cha baba yake. Watu wa Daudi walipofika kwa Hanuni katika nchi ya Waamoni ili kumfariji,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Daudi akawaza, “Nitamtendea wema Hanuni mwana wa Nahashi, kwa sababu baba yake alinitendea wema.” Hivyo Daudi akatuma wajumbe ili kumfariji Hanuni kwa ajili ya kifo cha baba yake. Watu wa Daudi walipofika kwa Hanuni katika nchi ya Waamoni ili kumfariji,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Daudi akasema, Nitamtendea wema Hanuni, mwana wa Nahashi, kwa kuwa babaye alinitendea mimi wema. Basi Daudi akatuma wajumbe ili kumtuliza kwa habari za babaye. Wakaja watumishi wa Daudi katika nchi ya wana wa Amoni kwa Hanuni, ili wamtulize.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Daudi akasema, “Nitamtendea mema Hanuni mwana wa Nahashi, kwani baba yake alinitendea mema pia.” Hivyo Daudi alituma wajumbe na kumpelekea salamu za rambirambi kwa ajili ya kifo cha baba yake. Nao wakaenda kwa Hanuni ili kumfariji, huko katika nchi ya Waamoni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Dawidi akasema: Nitamfanyizia Hanuni, mwana wa Nahasi, mambo ya upole, kwani baba yake alinifanyizia nami mambo ya upole. Kwa hiyo Dawidi akatuma wajumbe, wamtulize moyo kwa ajili ya baba yake. Lakini watumishi wa Dawidi walipofika katika nchi ya wana wa Amoni kwake Hanuni, wamtulize moyo,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Daudi akasema, Nitamtendea wema Hanuni, mwana wa Nahashi, kwa kuwa babaye alinitendea mimi wema. Basi Daudi akapeleka wajumbe ili kumtuliza kwa habari za babaye. Wakaja watumishi wa Daudi katika nchi ya wana wa Amoni kwa Hanuni, ili wamtulize.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Daudi akasema: “Nitamutendea mema Hanuni mwana wa Nahasi, maana baba yake alinitendea mema vilevile.” Halafu Daudi akatuma wajumbe na kumupelekea salamu za pole kwa ajili ya kifo cha baba yake. Nao wakaenda kwa Hanuni kwa kumufariji, kule katika inchi ya Waamoni.