1 Chronicles 19:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini viongozi wa Waamoni wakamwambia mfalme, “Je! Unadhani ni kwa sababu ya heshima ya baba yako ati Daudi ametuma wajumbe hawa waje kukufariji? Watu hawa si majasusi waliotumwa kuja kuichunguza nchi kuiangamiza na kuipeleleza?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
wakuu wa Waamoni wakamwambia Hanuni, “Hivi unadhani Daudi anamheshimu baba yako kwa kuwatuma wajumbe kukufariji? Je, hawa watu hawakuja kuipeleleza na kuidadisi nchi ili waishinde?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini wakuu wa wana wa Amoni wakamwambia Hanuni, Je! Waona Daudi amheshimu babayo kwa kukupelekea wafariji? Je! Hawakukujia watumishi wake ili kuiangalia nchi, na kuiangamiza, na kuipeleleza?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini viongozi wa Waamoni wakamwambia mfalme, “Je! unadhani ni kwa sababu ya heshima ya baba yako ati Daudi ametuma wajumbe hawa waje kukufariji? Watu hawa si majasusi waliotumwa kuja kuichunguza nchi kuiangamiza na kuipeleleza?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
wakuu wa Waamoni wakamwambia Hanuni, “Hivi unadhani Daudi anamheshimu baba yako kwa kuwatuma wajumbe kukufariji? Je, hawa watu hawakuja kuipeleleza na kuidadisi nchi ili waishinde?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
wakuu wa Waamoni wakamwambia Hanuni, “Hivi unadhani Daudi anamheshimu baba yako kwa kuwatuma wajumbe kukufariji? Je, hawa watu hawakuja kuipeleleza na kuidadisi nchi ili waishinde?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini wakuu wa wana wa Amoni wakamwambia Hanuni, Je! Unadhani Daudi amewatuma wafariji kwako kwa heshima ya baba yako? Je! Hawakukujia watumishi wake ili kuichunguza nchi, na kuiangamiza, na kuipeleleza?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini viongozi wa Waamoni wakamwambia mfalme, “Je! Unadhani ni kwa sababu ya heshima ya baba yako ati Daudi ametuma wajumbe hawa waje kukufariji? Watu hawa si majasusi waliotumwa kuja kuichunguza nchi kuiangamiza na kuipeleleza?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
wakuu wa wana wa Amoni wakamwambia Hanuni: Je? Dawidi anataka kweli kumheshimu baba yako machoni pako akituma kwako wajumbe wa kukutuliza moyo? Watumishi wake hawakuja kwako kuichunguza nchi na kuifudikiza na kuipeleleza?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini wakuu wa wana wa Amoni wakamwambia Hanuni, Je! Waona Daudi amheshimu babayo kwa kukupelekea wafariji? Je! Hawakukujia watumishi wake ili kuiangalia nchi, na kuiangamiza, na kuipeleleza?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini viongozi wa Waamoni wakamwambia mufalme: “Unazani ni kwa sababu ya heshima ya baba yako ndiyo maana Daudi anatuma wajumbe hawa wakuje kukufariji? Watu hawa ni wapelelezi waliotumwa kuja kuichunguza inchi kwa kuiangamiza na kuipeleleza.”