1 Chronicles 19:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
nao wakaondoka kurudi makwao. Daudi alipopashwa habari jinsi walivyotendewa wajumbe wake, alituma watu kuwalaki kwani hao wajumbe waliona aibu sana. Naye mfalme aliwaambia, “Kaeni mjini Yeriko, hata mtakapoota ndevu, Kisha mrudi.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mtu mmoja alipofika na kumpasha Daudi habari za watu hawa, akawatuma wajumbe wengine kuwalaki, kwa maana walikuwa wamevunjiwa heshima sana. Mfalme akasema, “Kaeni huko Yeriko hadi ndevu zenu ziote, ndipo mje.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakaenda watu wakamwambia Daudi jinsi walivyotendewa wale watu. Naye akatuma watu kuwalaki; kwa sababu watu hao walikuwa wametahayarika sana. Mfalme akasema, Ngojeni Yeriko, hata mtakapoota ndevu zenu, ndipo mrudi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
nao wakaondoka kurudi makwao. Daudi alipopashwa habari jinsi walivyotendewa wajumbe wake, alituma watu kuwalaki kwani hao wajumbe waliona aibu sana. Naye mfalme aliwaambia, “Kaeni mjini Yeriko, hata mtakapoota ndevu, Kisha mrudi.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mtu mmoja alipofika na kumpasha Daudi habari za watu hawa, akawatuma wajumbe wengine kuwalaki, kwa sababu waliaibishwa sana. Mfalme akasema, “Kaeni huko Yeriko mpaka ndevu zenu ziote, ndipo mrudi.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mtu mmoja alipofika na kumpasha Daudi habari za watu hawa, akawatuma wajumbe wengine kuwalaki, kwa maana walikuwa wamevunjiwa heshima sana. Mfalme akasema, “Kaeni huko Yeriko mpaka ndevu zenu ziote, ndipo mje.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo wakaondoka. Watu walipomwambia Daudi jinsi wajumbe wake walivyotendewa, alituma watu kuwalaki; kwa sababu walikuwa wameaibishwa sana. Mfalme akasema, Ngojeni Yeriko, hadi mtakapoota ndevu zenu, ndipo mrudi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
nao wakaondoka kurudi makwao. Daudi alipopashwa habari jinsi walivyotendewa wajumbe wake, alituma watu kuwalaki kwani hao wajumbe waliona aibu sana. Naye mfalme aliwaambia, “Kaeni mjini Yeriko, hata mtakapoota ndevu, Kisha mrudi.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
wakaenda zao. Watu walipompasha Dawidi habari za hao watu, akatuma wengine kuwaendea njiani, kwa kuwa watu hao walikuwa wametwezwa sana; mfalme akawaambia: Kaeni Yeriko, mpaka ndevu zenu zikue tena, kisha rudini!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakaenda watu wakamwambia Daudi jinsi walivyotendewa wale watu. Naye akatuma watu kuwalaki; kwa sababu watu hao walikuwa wametahayarika sana. Mfalme akasema, Ngojeni Yeriko, hata mtakapoota ndevu zenu, ndipo mrudi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
nao wakaondoka na kurudi kwao. Daudi alipopashwa habari jinsi wajumbe wake walivyotendewa, akatuma watu kwa kuwapokea maana wale wajumbe waliona haya sana. Naye mufalme akawaambia: “Mukae katika muji wa Yeriko, mpaka mutakapoota ndevu, kisha murudi.”